26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

TB Joshua Jr atoa siri ya kumshirikisha Walter Chilambo kwenye ‘Ni Wewe’

Na CHRISTOPHER MSEKENA

Mwimbaji wa Injili kutoka nchini Marekani, Daniel Badibanga maarufu kama TB Joshua Junior, amewashukuru wapenzi wa muziki huo kwa mapokezi mazuri ya wimbo wake, Ni Wewe aliomshirikisha Walter Chilambo.

TB Joshua Jr ambaye alizaliwa Julai, 1995 aliamua kujipa jina hilo kutokana na upendo wake kwa Nabii wa Kimataifa kutoka Nigeria, TB Joshua kwa kazi kubwa ya Mungu anayoifanya.

Akizungumzia sababu za kumshirikisha Walter Chilambo kwenye wimbo huo, TB Joshua Jr amesema: ” Nilimshirikisha Walter Chilambo kwenye wimbo wangu wa Ni Wewe kwasababu ni aina ya mwimbaji ambaye niliona atafiti kwenye wimbo huu.

” Ukiachana na umahiri wake wa kuimba, Walter ni ‘inspiration kwangu. Ni mtu ambaye historia yake ya hapo nyuma kama inafanana na yangu. Walter alikuwa akiimba nyimbo za Bongo Fleva hapo awali, baadaye akaja kuokoka na akaachana na Bongo Fleva akawa anaimba Injili hata mimi mwanzoni nilikuwa nafanya Hip hop baadaye nikaacha, nikaokoka nikaanza kuimba Injili kwahiyo huo ni mfano mmoja kati ya mingi kuhusu Walter,” amesema TB Joshua Jr.

Aidha mwimbaji huyo amesema ujumbe uliopo kwenye wimbo, Ni Wewe ni maisha halisi kabisa ya kumbukumbu za shukurani kwa Mungu.

“Ni kweli mimi nilitoka kwenye maisha ya kawaida kiasi kwamba nilijikuta sifai lakini Mungu hakunitupa alikuwa nami. Hebu nitizame leo, nimekuwa tofauti kabisa na mwanzoni. Haijalishi unapitia mangapi, usivunjike moyo. Ipo siku ya furaha vilevile unaweza ukadhani kwamba magumu unayoyapitia ni kwasababu ya dhambi zako au udhaifu wako sio kweli kabisa hakika Mungu ni wa ajabu sana, video tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube kila mtu anaweza kuitazama,” amesema TB Joshua Jr anayeishi Marekani kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles