25.5 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Tausi Likokola azindua kipindi chake cha televisheni

image2Na FESTO POLEA

MWANAMITINDO aliyeng’ara katika anga za kimataifa kwa zaidi ya miaka 20, Tausi Likokola, amezindua kipindi chake cha televisheni kinachoitwa ‘Tausi Likokola’s African Princess Model Search’ ambacho leo kitaanza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kupitia TV1.

Tausi alisema kipindi hicho kitaonyesha vipengele tofauti katika maisha kuanzia maadili, ulimbwende, nidhamu na mambo mengine anayotakiwa mrembo kuyazingatia.

“Naamini kupitia kipindi hicho, nitaweza kuongeza uwezo wa msichana mmoja mmoja katika stadi za uongozi na uwezo wa kujitambua, kujikubali, kujiamini na kuwa na mawazo chanya ya kujifunza stadi za mawasiliano bora ambayo yatawafanya warembo ninaowashindanisha mikoa mbalimbali wafanikiwe katika maisha ya mitindo,” alisema Tausi.

Tausi anayeishi nchini Marekani kwa sasa yupo nchini kwa ajili ya miradi yake mbalimbali kupitia kampuni zake mbili za ‘Tausi and Friends for Life’ na ‘Tausi Dreams Ltd’ inayozalisha pafyumu za Tausi Dreams pamoja na nywele za binadamu zinazoitwa Tausi Beautiful You Hair pamoja na kutangaza vitabu vyake vinne kikiwemo ‘The Art of the Beauty and Health’, ‘The African Princess’, ‘The Touch of an Angel’ na ‘Beautiful You’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles