21.9 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Tatizo la umeme Lindi, Mtwara laanza kutatuliwa

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SERIKALI imeanza kutatua changamoto za umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kuiunganisha mikoa hiyo kwenye umeme wa gridi ya taifa kupitia njia ya KV 400.

Akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Vedasto Ngombale (CUF), mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema suala la umeme kutoka Lindi hadi Mtwara lina changamoto nyingi za kiufundi linalopelekea tatizo hilo kijitokeza.

Alisema mitambo ya Somangafungu ina changamoto kwani umeme unaofuliwa katika mitambo hiyo unatumika katika wilaya za Kibiti, Kilwa na Rufiji ambapo hutumia Megawati 7.5 kwa kutumia gesi asilia.

Kutokana na hali hiyo, alisema Serikali kupitia Shirika la Umeme la Taifa (Tanesco) imeanza ukarabati katika wilaya za Kibiti, Kilwa na Rufiji wa mitambo miwili yenye uwezo wa kuzalisha umeme kwa jumla ya Megawati 5 unaotarajiwa kukamilika Novemba mwaka huu na utagharimu kiasi cha Sh bilioni tatu  ambapo ufufuaji wa mtambo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2.5 unategemewa kuanza Oktoba mwaka huu.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani, alisema Serikali imeanza utekelezaji wa ujenzi wa njia ya umeme itakayounganisha wilaya za Liwale na Nachingwea ambapo kwa sasa zinatumia umeme kutoka kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kilichopo Mtwara.

Naibu waziri huyo alisema hatua iliyofikiwa kwa mpango huo ni ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa KV 33 yenye urefu wa kilomita 14.5 kutoka Nachingwea hadi kijiji cha Luponda na kilomita 73 kutoka Liwale hadi Kijiji cha Nangano kuelekea Nachingwea.

Mbali na hayo, Tanesco inaendelea na ukaguzi, usafirishaji na ukarabati wa miundombinu ya kusambaza umeme kwa lengo la kuwaondolea wananchi kero ya kukatika kwa umeme, hatua itakayoondoa tatizo katika maeneo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,719FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles