Na Amina Omari,Tanga
TATIZO la udumavu mkoani Tanga, limepungua kutoka asilimia 39 mwaka janahadi kufikia asilimia 34.9 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kikao kazi cha maofisa lishe ngazi ya jamii jana,Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa alisema mikakati ya kupunguza udumavu umesaidia kuanza kupata matokeo ya haraka.
Alisema uwapo wa maofisa lishe hadi ngazi ya jamii, umesaidia kubaini watoto wenye utapiamlo mapema na kuwaanzishia tiba.
“Lishe ni jambo muhimu katika ukuwaji wa mwili na akili,ukosefu unaweza kuleta athari kwa mtoto na jamii,”alisema.
Aliwataka maofisa kuhakikisha wanafanyakazi ya kuwatambua watoto wenye utapiamlo mlo ngazi yajamii .
Ofisa Lishe Jiji la Tanga, Sakina Magadi alisema uwapo wa bajeti umesaidia kwa kiasi kikubwa kutekeleza afua za lishe.
“Mwaka jana pekee, tulingewa bajeti ya shilingi milioni 46 ambazo zimefanya shughuli mbalimbali, ikiwamo kuwajengea uwezo maofisa wetu ngazi ya jamii”alisema Magadi.
Alisema wasimamizi wameweza kuwa msaada mkubwa kuwatambua kwa wakati watoto wenye utapiamlo mlo na kuwasaidia tiba mapema.