29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

TASNIA YA FILAMU INAWEZEKANA KUFIKA ILIPO BONGO FLEVA

ZAMARADI

NA GRACE SHITUNDU

TASNIA ya filamu nchini Tanzania imeonekana ikididimia katika miaka ya hivi karibuni ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na ushindani mkubwa uliofanya sanii hii isonge mbele ka wakasi.

Dalili nyingi zimeendelea kujitokeza zikionyesha wazi tasnia ya filamu ikiendelea kuporomoka kutokana na kutokuwapo kwa uzalishaji wa kazi bora zinazoweza kukidhi matakwa ya soko la ndani na nje ya nchi.

Katika kudhihirisha hilo wasanii wengi maarufu ambao walitengeneza majina yao kupitia filamu kipindi hicho soko limechangamka hatuwaoni tena kama ilivyokuwa awali kitu kinachofubaza majina yao na kuididimiza tasnia kwa ujumla wake.

Hivi sasa wengi wao wamewekeza nguvu zao kwenye mitandao ya kijamii kwa kutupia picha za matukio mbalimbali ili tu wasotoke kwenye macho ya watanzania.

Siyo ajabu kuona mtu anayejiita staa wa filamu harafu mwaka mzima hajatoa filamu yoyote ila anaishi kwenye mitandao ya kijamii.

Wakati wengine wakiendelea kuishi maisha ya kuigiza kwenye mitandao baadhi yao wameamua kujirudisha kwenye tamthilia zinazoonyeshwa katika vituo vya mbalimbali vya runinga.

Najua kuna changamoto nyingi wanazokutana nazo wasanii wetu wa kitanzania ambazo ni pamoja na kunyonywa na wasambazaji sambamba na wizi wanaofanyiwa na wanaorudufu kazi zao kitu kinacho wakatisha tamaa.

Matatizo hayo yanashughulikiwa kwa kuwa yalikuwapo kitambo na sanaa ilikuwa inasonga mbele na kwa maana hiyo tatizo la kuporomoka kwa tasnia limesababishwa na wasanii wenyewe.

Huu ni Mwaka mpya wasanii wa filamu na maigizo nchini mnapaswa kujitafakari kwa kina mlikosea wapi na mfanye nini ili muweze kufanya kazi zitakazoweza kuipeperusha bendera yetu.

Mnapaswa kubadilika katika kazi zenu na katika maisha ya kwaida,  acheni kuishi maisha ya kuigiza bali igizeni katika kazi ambazo zitaweza kuwaingizia kipato na faida zaidi.

Mkubali kujifunza, kwani njia za kujifunza kwa zama hizi za teknolojia zimerahisishwa kwa kiwango cha juu pasipo kujiona kuwa ni msanii mkubwa au chipukizi.

Mna lugha ya Kiswahili ambayo ni silaha kubwa ya kuweza kupenya katika nchi za Bara la Afrika na Ulaya inayotumiwa na baadhi ya wasanii wa nchi jirani.

Pambaneni mpate sera ya filamu ambayo itatekelezeka ili tasnia hii eweze kutoa ajira kwa vijana wengi zaidi na kufikia mafanikio waliyonayo wasanii wa muziki wa Bongo Fleva.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles