21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

TASAF WAKOMBOA FAMILIA ZILIZOKIMBIWA NA WENZA WAO

 

Na Derick Milton, Meatu

“HAKUNA jambo linaloniumiza kama kuona watoto wangu wakishinda au kulala bila ya kula. Kuna wakati niliwakataza kwenda shule ili wanisaidie kulima vibarua, tupate chakula na fedha ya kununua mahitaji mengine.”

Hii ni kauli ya Richald Ruhela mkazi mkazi wa Kijiji cha Mwambiti, Kata ya Mwamishali iliyoko Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.

Ruhela (53) anasema miaka 20 iliyopita alifunga ndoa na Elzabeth Mathias na kufanikiwa kupata watoto watano.

Anasema licha ya kwamba walikuwa wakiishi kwenye nyumba za kupanga, maisha yao hayakuwa mabaya kwa kuwa walipenda kujishughulisha wakifanya biashara ya duka na kulima.

“Tulikuwa tunakodi mashamba tunalima, tukivuna tunauza baadhi ya mazao na mengine tunahifadhi kwa ajili ya chakula, maisha yalikuwa mazuri kutokana na kuishi kwa furaha na amani,” anasimulia Ruhela.

Richard anasema licha ya changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo, bado walipambana kuwapatia watoto wao mahitaji yote ya shule.

Anasema ilipofika mwaka 2012 mkewe akamkimbia na hapo ndipo maisha yalianza kubadilika kwani kulea watoto peke yake haikuwa kazi rahisi.

Ruhela anasema hali ilivyozidi kuwa ngumu alilazimika kuwaachisha shule ili wasaidiane kulima vibarua na kupata chakula.

“Kisa cha mke wangu kunikimbia ni madai kwamba ameshindwa kuishi maisha tuliyokuwa tukiishi – ya umaskini.

“Baada ya muda nilipata taarifa kuwa alikuwa akiishi na mwanamume mwingine mwenye uwezo kifedha,” anasema na kuongeza:

“Maisha kwa upande wangu yalikuwa magumu mno, kuna wakati nilitamani kutoweka duniani. Kula yangu ilikuwa ni ya shida, nilifikia hatua ya kuomba msaada kijiji kizima.

Alibuto Jilasa ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwambiti, anakiri ofisi yake kupokea maombi kutoka kwa Ruhela akitaka asaidiwe chakula na mahitaji mengine kwa ajili ya watoto wake.

Jilasa anasema serikali ya kijiji iliona kuna umuhimu wa kumsaidia hivyo wakampatia kilo 100 za mahindi, fedha taslimu kwa ajili ya kusaga unga na kununua mboga na mahitaji mengine.

Eliwaza Reuben ni Mkazi wa Kijiji cha Mwamishali, Kata ya Mwamishali, historia ya maisha yake haitofautiani na Ruhela.

Anasema mwaka 2010 mume wake alimkimbia kutokana na maisha ya kimaskini waliyokuwa wakiishi.

Anasema awali aliishi na mume wake, Jacob Reuben, maisha ya kawaida, ambapo walikuwa wanajihusisha na kazi za kulima mashamba ya kukodi.

“Wakati mwingine tulilazimika kufanya vibarua kwenye mashamba ya watu na kupata kipato cha kumudu majukumu ya kifamilia,” anasema Eliwaza.

Anasema maisha yalianza kubadilika baada ya mumewe kumtelekeza, hivyo akalazimika kuwaachisha wanawe shule.

 

Tasaf wawanusuru

Mpango wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu (TASAF III), ndiyo mwokozi wa familia ya Ruhela na Reuben.

Ruhela anasema kutokana na maisha kuzidi kuwa magumu uongozi wa kijiji ulimwingiza katika mpango TASAF kusaidia kaya masikini na hivyo kuanza kupewa fedha Sh 48,000 kila baada ya miezi miwili.

Anasema kiasi hicho cha fedha kilimwezesha kuanza kufuga mbuzi na kukodi mashamba kwa ajili ya kilimo.

“Nilianza kufuga mbuzi watatu, lakini hadi sasa nina mbuzi 40 wakubwa na wadogo, wengine nimeanza kuwauza na sasa nimejenga nyumba ya kuishi,” anasema na kuongeza:

“Nyumba niliyojenga ni ya nyumba vinne na tayari ina umeme, watoto nao sasa wanakwenda shule bila tatizo lolote,” anasema Ruhela.

Kwa upande wake Reuben naye alifanikiwa kupata msaada kutoka TASAF na sasa anamudu kusomesha watoto na tayari ameshanunua kiwanja kwa ajili ya kujenga nyumba ya kuishi.

“Huwa napewa Sh 72,000 kutoka TASAF, fedha ambazo zilinisaidia kukodi mashamba na kuanza kulima mazao ya chakula na biashara,” anasema Reuben.

Anasema sasa hivi mwanawe wa kwanza, Joseph Jacob yupo chuo kikuu na wa pili, Rahali Jacob anasoma kidato cha sita.

 

Mkuu wa wilaya

Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Joseph Chilongani, anasema kupitia mpango huo jumla ya kaya 4,892 zilizoko kwenye mpango, zimefanikiwa kuanzisha miradi mbalimbali inayowaingizia kipato.

Anasema kaya hizo zimefanikiwa kuondokana na nyumba za tende, huku zikijuhusisha na ufugaji wa ngo’mbe, mbuzi, kondoo, kuku, bata na nguruwe. Pia wanajihusisha na kilimo cha pamba na mazao mengine.

Anasema hadi sasa mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Meatu umetoa Sh bilioni 4.1 katika vijiji 69.

 

Mratibu wa TASAF

Mratibu wa mpango huo wilayani hapa, Rajabu Juma, anasema hali ya familia zilizoko kwenye mpango huo zimebadilika kwa kiwango kikubwa.

Anasema familia nyingi sasa hivi zinamudu maisha

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles