25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

TASAF kuandikisha walengwa kidigitali

Florence Sanawa, Mtwara

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF),  Ladislaus Mwamanga amesema kuwa mfuko huo utaanza kufanya uandikishaji walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini kidigitali. 

Awali mwanzo wa mradi huo ilionyesha wananchi wengi wenye sifa waliingia kimakosa huku wenye sifa wakiachwa hatua ambayo imeifanya TASAF kuja na maboresho ya kidigital ili kupunguza udanganyifu. 

Akizungumza katika kikao kazi cha majaribio ya kuimarisha utambuzi na uandikishaji kwa kaya masikini katika halmashauri ya Mji Nanyamba na Wilaya ya Mtwara  mkoani Mtwara alisema mpango huo utasaidia kupunguza udanganyifu na kuwasaidia kupata taarifa sahihi ya kaya hizo. 

Alisema kuwa wamekuwa na utaratibu huo maalum ili kuwawezesha kupata taarifa na vigezo sahihi kwa walengwa wa mpango huo na wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu na serikali ya Zanzibar pamoja na Ofisi ya Takwimu ya Taifa ili kuwa na takwimu sahihi ya ujumla ya kaya masikini. 

Aidha alisema mpango huo unajaribu kuupitia upya mfuko na kuuimarisha kwa utambuzi na uandikishaji wa walengwa kwa njia sahihi itakayokwepesha udanganyifu. 

Nae Mkuu wa wilaya ya mtwara Evod Mmanda alisema kuwa  wawezeshaji wa mfuko wa TASAF wana nafasi ya kuelimisha wananchi juu ya kujiinua kiuchumi ili waache kulilia umasikini wanapokosa sifa za kuwepo kwenye mpango huo. 

Mmanda alisema endapo wananchi watapewa elimu juu ya kufanya kazi ili kuondokana na umasikini itasaidia kupunguza idadi ya kaya masikini. 

“Wananchi wanapaswa wajue kuwa huu mfuko sio wakudumu ni sehemu tu ya kuwavusha ili watoke sehemu moja kwenda nyingine ndiyo maana tunawahamasisha kushiriki vikoba ili kujiwekea akiba lakini pia kufanya biashara mbalimbali, ufugaji na kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi,” alisema. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara,  Mussa Ndazigula alisema kuwa uandikishaji huo utapunguza maswali kutoka kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles