26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

TAS yaomba Halmashauri nchini kutenga bajeti kwa ajili ya kuwasaidia mafuta kinga

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Chama cha Watu wenye Ulemavu wa ngozi (TAS) kimetoa wito kwa Serikali kuhakikisha Halmashauri zinatenga bajeti ya kutosha ili kuwasaidia kupata mafuta kinga sambamba na kuboresha vitengo vya kupima saratani ya ngozi ili kuwawezesha kutibiwa kwa wakati na kupunguza mwendo wa kufata huduma.

Wito huo umetolewa na Juni 13, mwaka huu na Afisa Huduma kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi, Christina Silas, wakati akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasimi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja. Gen Charles Mbuge kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa, katika kilele cha Maadhimisho ya kujenga Uelewa kwa watu wenye uelemavu wa ngozi yaliyofanyika Kitaifa mkoani Kagera.

Kwa mujibu wa chama hicho, siyo watu wote wenye ulemavu wa ngozi ambao hufikiwa na msaada wa mafuta kinga ambayo yanakinga ngozi zao na saratani, nakwmaba ni wachache tu ndio hupata huduma hiyo ambayo utolewa na wahisiani katika vituo mbalimbali wanavyoishi.

“Ni Mikoa michache na halmashauri chache ambazo hutenga bajeti kwa ajili ya huduma ya kuwapatia mafuta kinga watu wenye ulemavu wa ngozi, pia kuna umbali mrefu juu ya kuchunguza afya zao katika kuhakikisha wale wanaopata saratani wanapata huduma,” amesema Silas.

Aidha, wameomba mabadiliko ya Sheria na kanuni katika asilimia 2 kati ya 10 ya mikopo ya halmashauri ambayo inayotolewa kwa watu wenye ulemavu kuwa imekuwa ikinufaisha vikundi vichache kinyume na uhalisia hivyo mabadiliko yalenge kuwashirikisha watu wenye ulemavu.

Katika hatua nyingine wamepongeza hatua mbalimbali za serikali ambazo imechukua katika kuelimisha jamii juu ya kukabiliana na unyanyapaa.

“Kuna hatua kubwa imefanyika ikilinganishwa na miaka 10 nyuma katika ngazi za kupata usawa mfano elimu, huduma za afya, kushika nafasi za kiasiasa, kuchangamana, kushiriki ngazi ya maamuzi pamoja na miundombinu iliyopo shuleni na vituo vya afya,” amesema.

Upande wake, Meja General Charles Mbuge amesema serikali inaendelea kuboresha sehemu za upatikanaji huduma hasa kitengo cha kupima saratani ya ngozi za watu wenye ulemavu wa ngozi kuhakikisha wanaendelea kupata huduma bora na kuondokana na unyanyapaa katika jamii.

Amesema kwa mwaka 2021 pekee watu wenye ulemavu wa ngozi wapatao 241 wameajiliwa huku mafuta ya kukinga ngozi yakitolewa na watu 3,600.

“Kwa sasa halmashauri 131 zinapata mafuta kinga bure, nisisitize halmashauri zote kuendelea kutenga bajeti za kununua mafuta na kuwafatilia kuhakikisha watu wenye ulemavu wa ngozi wanashiri katika maendeleo ya taifa,” amesema.

Maadhimisho ya kujenga uelewa juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi yameadhimishwa mkoani Kagera Juni 13, 2022 na kutoa huduma mbalimbali bure kama kupata chanjo ya Uviko-19, kupima saratani ya ngozi na kupata ushauri mbalimbali na elimu juu ya ulemavu wa ngozi unavyotokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles