30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Tarura Simiyu yaanza kukarabati barabara, madaraja yaliyoharibiwa na mvua

Derick Milton, Simiyu

Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini (Tarura) mkoani Simiyu wameanza kufanya matengenezo ya barabara na madaraja katika maeneo korofi yaliyoharibiwa na  mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.

Matengenezo hayo yatakayogharimu kiasi cha Sh bilioni 1.3 yatagusa ujenzi wa madaraja na barabara kwa asilimia 45 ya hali halisi ya kiwango cha barabara zote zisizopitika mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa Tarura mkoa, Mhandisi Kk. Philemon Msomba amesema mkoa huo una urefu wa barabara zenye kilometa 4038.16, zinazohudumiwa na tarura kati ya hizo asilimia 55 ziko vizuri na zinapitika bila shida.

Dk. Msomba amesema kwa sasa wameanza na ukarabati wa daraja la bunamhala katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Nyambuli lililopo Kata ya Dutwa kwa gharama ya Sh milioni 58 kwa kutumia fedha za dharura ambazo wamepata.

Ameongeza kuwa wameamua kuanza na madaraja hayo korofi ili kuwaondolea adha ya usafiri wananchi wa maeneo hayo ambao walikuwa wakilazimika kutengeneza madaraja ya miti.

“Tuliomba kupatiwa kiasi cha Sh. bilioni 1.3 kama dharura na serikali imeanza kutupatia hivyo ndani ya siku chache tutapewa fedha yote tuliyoomba, maeneo yote ambayo yamearibiwa na mvua ni asilimia 45 ya mtandao mzima wa barabara zetu, na zilizobaki zinapitika vizuri,” amesema Dk. Msomba.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles