28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

TAOMAC yakanusha mtafaruku na EWURA

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa mafuta nchini(TAOMC) kimekanusha taarifa za uvumi unaoenezwa mitandaoni kuwa kina mtafaruku na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Taarifa iliyotolewa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama hicho leo Alhamisi Julai 27, 2023 jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa hakijafanya kikao na EWURA kwa wiki mbili sasa.

“Tumebaini kuwepo kwa taarifa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ikidai kuwa waagizaji na wasambazaji wa mafuta wamekaa kwenye kikao na EWURA na kuishia kwenye mtafaruku na kutokukubaliana.

“Kwa niaba ya wanachama wetu, wa Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta Tanzania (TAOMAC) ambao wanajumuisha zaidi ya asilimka 97 ya soko la mafuta yanayoingizwa nchini, yunapenda kukanusha taarifa hizi kwa kuwa sio za kweli.

“Hatujaakaa kikao na EWURA kwa zaidi ya wiki mbili. Pia hatujawahi kukaa kikao na EWURA na kuishia kwenye mtafaruku,” imeeleza taarifa ya chama hicho.

Katika hatua nyingine taarifa hiyo ya TAOMAC imeeleza kuwa sekta ya uagizaji na usambazaji wa mafuta inapitia changamoto ya ukosefu wa dola.

“Lakini tumeshakaa vikao na mamlaka zinazohusika na tumeahidiwa kuwa tatizo hilo linafanyiwa ufumbuzi.

“Wanachama wetu wanaendelea kuagiza mafuta na wataendelea kufanya hivyo, ili kuhakikisha nchi haikosi mafuta,” imeeleza taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles