26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yatoa uhalali wa kampuni kwa Burundi

Benjamin Masese – Dar es Salaam

SERIKALI ya Tanzania imewahakikishia wajumbe 11 wa kamati teule ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwamba wanaitambua Kampuni ya Mbogo Kampuni ya Mbogo  Mining & General Supply Ltd na shughuli zote inazofanya  nchini ni halali.

Kauli hiyo imetolewa  na baadhi ya mawaziri akiwamo  Waziri wa Madini, Doto Biteko , Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro katika vikao  vilivyofanyika kwa nyakati tofauti na wajumbe hao.

Rais Nkurunzinza aliteua kamati hiyo kuja Tanzania  na kukutana na viongozi wa Serikali ili kupata  taarifa sahihi  na uhalali wa kampuni hiyo ambayo inatarajiwa kukabidhiwa jukumu la  kusambaza vilipuzi nchini Burundi sambamba  na kushiriki mkutano wa kimataifa wa uwekezaji  katika sekta ya madini.

Akizungumza na wajumbe hao, Biteko alisema  Serikali ya Tanzania haina shaka na kampuni hiyo na haijawahi kukiuka au kwenda kinyume na vibali vinavyotolewa na wizara, hivyo aliwataka kuondoa wasiwasi na kuipatia kazi nchini Burundi.

 “Tunashukuru kwa ujio wenu maana shughuli ambazo zinafanywa na kampuni hii ni nyeti na zinaweza kuhatarisha usalama wan chi, lakini niwahakikishie kwamba tunafahamu kila kitu juu ya Mbogo Mining kwanza haijawahi kuleta shida tangu tunaipa vibali.

“Hapa nimeambatana na watalaamu ambao kila siku wanafanya nao kazi hivyo nawapa uhuru wa kuhoji kila kitu mnachotaka na majibu yatapatikana,” alisema

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda , Manyanya ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Riziki Shamdoe na watalaamu wengine alisema  hawana wasiwasi na kampuni hiyo na inafahamika serikalini na wanashirikiana katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

“Mbogo Mining imeweka historia hapa nchini kwa namna inavyowekeza na hadi nje ya nchi, kitendo cha kufika kwenu Burundi  kimetuunganisha zaidi katika sekta ya viwanda na biashara na shughuli hii bila shaka itaongeza ajira kwa mataifa haya mawili,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles