24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yatakiwa kuimarisha uhusiano

minjaNa Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

SERIKALI imetakiwa kuimarisha ushirikiano wa kibishara baina ya nchi tano ambazo zinategemea bandari ya Tanzaia ili kukuza uchumi wa Taifa.

Mbali na hilo, Serikali imetakiwa kutengeneza mfumo wa hiari katika ulipaji kodi za ndani ili kuhakikisha  hakuna watu wanaokwepa kodi.

Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Jonson Minja alisema ni vyema Serikali ikatengeneze mazingira mazuri ya kibiashara baina ya nchi hizo.

Alizitaja nchi hizo, kuwa ni Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia na Malawi.

“Ni vyema Serikali ihakikishe inatengeneza mazingira mazuri ya kibiashara baina ya nchi hizi. Mfano mzuri ni namna Serikali ilivyotushirikisha wafanyabiashara  kuweka bei elekezi ya malipo na makontena katika Bandari ya Dar es Salaam.

“Sote tumeona matokeo mazuri yamejitokeza, mwezi uliopita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilikusanya Sh trioni 1.4 kiasi ambacho hakijawahi kutokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles