24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yatajwa kupunguza upatikaji dawa za kulevya

Christina Gauluhanga – Dar es Salaam

TANZANIA imetajwa kuwa moja ya nchi chache barani Afrika zilizofanikiwa kupunguza upatikanaji na uhitaji wa dawa za kulevya kwa asilimia 90, hususan heroin zilizokuwa zinaingia kupitia ukanda wa bahari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu Kamishna Jenerali wa Dawa za Kulevya nchini (DCEA), James Kaji alisema mafanikio hayo ya Tanzania yalibainishwa katika mkutano wa 63 wa Kamisheni ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (CND 63), uliofanyika Vienna, Australia.

Alisema kuwa kwa kiwango kikubwa wamefanikiwa kupunguza madhara yanayosababishwa na dawa hizo, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuwekeza mikakati ya kupambana na tatizo hilo kwa uwiano ulio sawa.

“Tuna kila sababu kama nchi au mamlaka kujipongeza, kwa sababu Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia dawa za kulevya na uhalifu (UNODC), kupitia CND limeipongeza Tanzania kwa jitihada na kuleta matokeo chanya katika mapambano dhidi ya dawa hizo duniani,” alisema Kaji.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu, yaani 2018 hadi 2020 wamefanikiwa kuhakikisha wanatokomeza matumizi ya dawa hizo.

Kaji alisema mafanikio hayo yamekuja kwa sababu ya jitihada za Serikali kufanya marekebisho makubwa kwa kutunga Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya Sheria No.5 ya mwaka 2015 na mabadiliko yake ya mwaka 2017 kwa Tanzania Bara na Visiwani mwaka 2019.

Licha ya hali hiyo, alisema kuwa wamefanikiwa kudhibiti mipaka yote ya ukanda wa bahari ambapo wamekuwa wakishirikiana na vyombo vingine kuimarisha ulinzi kwa kufanya doria za mara kwa mara.

Kaji alisema mafanikio hayo ndiyo yaliyowapa heshima mwaka jana ya kuandaa mkutano wa 28 wa UNODC ambao ni wa Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Afrika wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na tatizo la dawa za kulevya (Honlea 28), uliofanyika Dar es Salaam.

Kaji alitumia fursa hiyo kuviomba vyombo vya habari kuandika habari za kina na zenye utafiti kuhusu mamlaka hiyo na kuvitaka kuacha kutumika na watu wa mataifa mengine kuichafua mamlaka hiyo kwa sababu vita hiyo ni ya taifa zima.

Alisema Tanzania ni moja ya nchi zilizopata mafanikio na hata nchi za Ghana, Uganda, Msumbiji, Nigeria na Norway wameomba kujifunza mfumo wa utendaji kazi pamoja na sheria inavyofanya kazi hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles