27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TANZANIA YASAINI MKATABA WA BIL 60/- UFUNGAJI RADA

NA CHRISTINA GAULUHANGA

DAR ES SALAAM

SERIKALI ya Tanzania na Kampuni ya M/S Thales Air System kutoka nchini Ufaransa imesaini mkataba wa ufungaji wa mitambo minne ya rada itakayogharimu Sh bilioni 61.3.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo na uzinduzi wa nembo mpya ya mamlaka, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari alisema mamlaka hiyo itagharamia mradi huo kwa asilimia 45 na Serikali Kuu itatoa asilimia 55.

Alisema mchakato wa ununuzi wa rada, uliadhimiwa mwaka jana na wafanyakazi kwa kutumia mapato ya ndani baada ya kuona  iliyopo sasa imepunguza uwezo.

“ Ni imani yetu manunuzi ya rada hizi yatasaidia kuona anga lote hapa nchini tofauti na sasa ambapo baadhi ya maeneo hayaonekani vizuri,”alisema Johari.

Alisema ongezeko la ndege zinazotumia anga la Tanzania, limesababisha kuwa na mahitaji ya mitambo ya kisasa ili kufanikisha urukaji ndege kwa kufuata viwango vya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

Alisema ndege zikipita futi 24,500 za hapa nchini haziwezi kuonekana,  endapo rada hizo zitafungwa zitakuwa na uwezo mkubwa wa kuona anga nzima.

Alisema mradi huo, utachukua miezi 18 ambapo rada zitafungwa  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Mwanza, Kilimanjaro  (KIA) na Uwanja wa Ndege wa Songwe.

Alisema rada hizo zitasaidia kuongeza usalama wa anga  na kuongeza mapato yatokanayo na tozo ya ndege zinazopita katika anga ya Tanzania.

“Kwa kutumia mawasiliano ya radio mwongoza ndege analazimika kutenga au kupanga dnege moja na nyingine kwa maili 80 ili ziende kwa usalama ambapo kwa kutumia rada mwongoza ndege atapanga ndege nane kwenye umbali huo,”alisema Johari.

Alisema uboreshwaji wa miundombinu hiyo, utavutia ndege nyingi zaidi kupita na kuendesha shughuli zake katika anga la Tanzania.

Alisema hadi sasa wafanyakazi 33 wa mamlaka hiyo, wameanza mchakato wa kujiendeleza kielimu ili uendesha mitambo ya rada hizo.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa aliwataka wasimamizi wa mradi huo kuwa waadilifu katika ufungaji wa rada.

Alisema endapo mkandarasi aliyepewa kazi hiyo hatatimiza vigezo vinavyotakiwa wasikubali kuendelea naye.

Alisema rada hizo zikifungwa zitasaidia kuona ndege zinazopenya kinyemela katika baadhi ya migodi na mbuga  za wanyama, ambapo hata serikali itakusanya mapato yake kwa usahihi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles