33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yapiga hatua utoaji wa mikopo ya Nyumba

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Tanzania imepiga hatua katika utoaji mikopo ya nyumba ambapo jumla ya mikopo 6,182 imetolewa hadi sasa ikilinganishwa na mikopo 579 iliyotolewa kufikia mwaka 2009

Aidha, muda wa urejeshaji mikopo umeongezeka kutoka miaka 15 hadi 25 sambamba na riba ya mkopo kupungua kutoka asilimia 20 – 22 mwaka 2009 hadi asilimia 15-19 zinazotozwa sasa.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula (katikati) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 41 wa Taasisi ya Shelter Afrique unaofanyika katika mji wa Victoria Falls, Zimbabwe.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula Julai 27, 2022 katika Mkutano Mkuu wa 41 wa Taasisi ya Shelter Afrique unaoendelea kwenye Mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe ambapo Tanzania inahudhuria kama mwanachama wa Taasisisi hiyo.

Akichangia mada kuhusu jukumu la Benki Kuu kwenye soko la nyumba katika Bara la Afrika huku akitoa uzoefu wa Taasisi ya ‘Tanzania Mortage Refinance Company’ iliyoanzishwa kufuatia utekelezaji wa mradi wa mikopo ya nyumba uliokuwa ukisimamiwa na Benki Kuu, Dk. Mabula alisema kumekuwa na mafanikio makubwa toka kuanzishwa taasisi hiyo ambapo kwa sasa jumla ya Benki na Taasisi za fedha 33 zinatoa mikopo ya nyumba tofauti na ilivyokuwa kabla ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ambapo benki 3 tu ndizo zilizokuwa zikitoa mikopo.

‘’Kumekuwa na mafanikio makubwa toka kuanzishwa Taasisi ya Tanzania Mortage Refinance Company ambapo kwa sasa jumla ya benki na Taasisi za fedha 33 zinatoa mikopo ya nyumba tofauti na ilivyokuwa kabla ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ambapo benki 3 tu ndizo zilizokuwa zikitoa mikopo,” alisema Dk. Mabula.

Hata hivyo, Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwaeleza washiriki wa mkutano huo umuhimu wa Benki Kuu kusimamia ipasavyo Benki na Taasisi zinazotoa mikopo hiyo ili kuhakikisha zinatoa riba ambazo wananchi wataweza kumudu kwa kuwa nazo zinawezeshwa kupata mitaji nafuu.

Akielezea upungufu wa nyumba 3,000,000 na mahitaji ya nyumba 200,000 kwa kila mwaka nchini Tanzania, Dk. Mabula alisema, endapo benki na taasisi za fedha zitaendelea kuachiwa kutoza riba kubwa bila usimamizi haitafanikiwa kuwezesha wananchi hususan wa kipato cha chini kumudu gharama za nyumba bora.

‘’Endapo benki na taasisi za fedha zitaendelea kuachiwa kutoza riba kubwa bila usimamizi haitafanikiwa kuwezesha wananchi hususan wa kipato cha chini kumudu gharama za nyumba bora,’’ alisema Dk. Mabula.

Mkutano Mkuu wa 41 wa Taasisi ya Shelter Afrique ulioanza Julai 25, 2022 unatarajiwa kumalizika kesho Julai 29, 2022 na unahudhuriwa na nchi wanachama wa Bara la Afrika ikiwemo Tanzania na umebeba kauli mbiu ya ‘Climate Change and the Built Environment’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles