26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Tanzania yakabiliwa na uhaba wa wataalamu sekta ya bahari

Ramadhan Hassan, Dodoma

Tanzania inauhaba wa wataalamu katika sekta ya bahari hali ambayo imekuwa ikiwalazimu kuwatoa nje ya Nchi.

Hayo yameelezwa Jumanne Machi 7,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Mkeyenge wakati alipokuwa akiyataja mafanikio ya Shirika hilo katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita,mbele ya Waandishi wa Habari.

Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa nchini kuna chuo kimoja cha Bahari hivyo wamekuwa wakiomba wataalamu kutoka nje ya nchi.

Amesema baadhi ya wataalamu watafika Machi mwaka huu na wengine Aprili na watatoa mafunzo ya ukoaji na utafutaji.

“Hawa wataalamu watatusaidia zaidi kutufundishia vijana wetu,hii ni sekta ya Kimataifa na sisi tuna uhaba wa wataalamu lazima tuwatoe nje,”amesema Mkeyenge.

Mkurugenzi huyo amesema wamesaini jumla ya mikataba 24 huku sita ikiwa ni ya lazima katika kuhakikisha sekta hiyo inazidi kuboreka.

Amesema jumla ya kaguzi 4,490 zimefanyika katika kipindi cha Julai 2022 hadi Januari 2023 huku wakitarajia kufikia vyombo takriban 8,000 ifikapo Juni 2023.

Aidha, amesema TASAC imekuwa ikiratibu Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kupambana na Umwagikaji wa Mafuta Baharini.

Mkenyenge amesema kwa kwa mwaka wa fedha 2021-2022 jumla ya vyeti 16,718 vya mabaharia vilitolewa.

Amesema katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 mpaka Januari 2023, Shirika liliweza kutoa vyeti 9,570 na takribani vyeti 17,000 vinavyotarajiwa kutolewa ifikapo Juni 2023.

Mkurugenzi huyo amesema Wakala umeweza kuongeza mchango katika Mfuko Mkuu wa Serikali, mwaka hadi mwaka kutoka Sh 9.1 bilioni katika mwaka wa fedha 2018/19 hadi kufikia Sh 43.5 bilioni katika mwaka wa fedha 2021-2022.

Amesema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 21 na hivyo kufanya jumla ya mchango wa TASAC katika mfuko mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miaka minne kuwa Sh bilioni 104.5.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,407FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles