26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yajivunia miaka 20 ya‘Beijing’

waziri simbaNa Mwandishi Maalum, New York
USHIRIKI wa askari wanawake katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa (UN) ni baadhi ya mafanikio ambayo Tanzania inajivunia miaka 20 baada ya mkutano wa historia wa wanawake uliofanyika Beijing, China mwaka 1995.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba aliyasema hayo juzi alipotoa tathmini na changamoto za utekelezaji wa maazimio muhimu yaliyofikiwa katika mkutano huo wa wanawake.
Waziri Simba ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Hadhi ya Wanawake ( CSW) jijini hapa ambao unajumuisha washiriki kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“Miaka 20 iliyopita yapo mambo mengi ambayo Tanzania tumepiga hatua za kuridhisha katika maeneo ya uwezeshwaji na fursa sawa kwa wanawake ambapo Katiba za pande zote mbili za Muungano zinaainisha vema kuhusu hadhi ya mwanamke.
“Katika Katiba mpya inayopendekezwa kuna eneo ambalo linazungumzia kwa kina usawa wa jinsia na uwezeshwaji wa wanawake.” alisema Waziri Simba.
Simba pia alizungumzia baadhi ya sheria ambazo ama zimefanyiwa marejeo au kutungwa kwa lengo la kuboresha usawa wa jinsia.
Alizitaja sheria hizo kuwa ni sheria zinazohusu watoto, usafirishaji wa binadamu, ardhi, HIV/AIDS na sheria ya makosa ya kujamiana.
Katika hotuba hiyo, Waziri Simba pia alisema kuanzishwa kwa dawati la jinsia na watoto katika vituo vya polisi kwa ajili ya watoto na wanawake wanaofanyiwa ukatili ni baadhi ya mafanikio ambayo Tanzania imeweza kupiga hatua nzuri zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles