23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yahitaji tril. 706/- kuboresha miundombinu

Na MWANDISHI WETU

IMEELEZWA kuwa, Tanzania inatumia dola za Marekani bilioni 206 (sawa na Sh trilioni   4.5) kwenye kujenga miundombinu yake,   huku mahitaji   kamili yakiwa ni dola bilioni 321 (sawa na Sh trilioni 706) hadi kufikia mwaka 2040.

Pamoja na hali hiyo, inatabiriwa kutegemea ukuaji wa kasi wa uchumi wenye wastani wa asilimia 6 kwa mwaka na pia ongezeko kubwa  la idadi ya watu lenye wastani  wa asilimia 2.9 kwa mwaka.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya mtazamo wa miundombinu duniani iliyotolewa jana jijini London, nchini Uingereza na Taasisi  ya   Global Infrastructure Hub (GIH), ambayo ni mojawapo ya huduma za nchi 20 zilizojikimu duniani (G20).

Ripoti hiyo ilibainisha kuwa, Tanzania itahitaji kutumia asilimia 21 ya Pato lake la Taifa (GDP) katika kujenga miundombinu yake ili iweze kufikia mahitaji yanayoendelea kukua na malengo ya maendeleo ya kudumu ya Umoja wa Mataifa, ambayo ni juu zaidi ikilinganishwa na wastani wa asilimia 7.7 iliyotumika kati ya 2007 na 2015.

Akizungumzia ripoti hiyo, Mkurugenzi   Mtendaji  wa Kituo cha Miundombinu Duniani (GIH), Chris Heathcote, alisema:  “Mtazamo huu ni mpana na wa uchambuzi wa kina wa mahitaji ya uwekezaji kwenye miundombinu ambayo inaipa nchi takwimu za matumizi ambazo serikali na wahisani zimekuwa zikihitajika.

Heathcote alikwenda mbali zaidi na kuelezea kuwa, mtazamo huu unatueleza vitu vikuu vitatu, ni kiasi gani nchi inahitaji kutumia kwenye miundombinu kuelekea 2040, wapi mahitaji hayo yanahitajika kwa kila sekta ya miundombinu, pengo ni la kiasi gani ukizingatia mwenendo wa matumizi yao kwa sasa.

Alisisitiza  kuwa, ili kufikia malengo  ya kudumu ya  maendeleo (SGDs), nyongeza  ya uwekezaji ya dola bilioni 57(Sh trilioni 1.3)  itahitajika katika sekta ya umeme, ikifanya jumla kwa yote kufikia dola bilioni 378 (sawa  na Sh trilioni 8.3).

Ripoti mpya ya kituo cha uwekezaji cha nchi za G20 inaelezea mahitaji ya uwekezaji kwenye miundombinu duniani kwa nchi binafsi 50 na sekta saba.

Pamoja na hali hiyo, ripoti hiyo inaeleza kuwa, gharama za kuweka miundombinu ili kusaidia ukuaji wa uchumi na kuanza kuziba mapengo kwenye sekta ya miundombinu, ikitabiriwa kufikia trilioni 94 ifikapo 2040, na nyongeza ya dola za Marekani trilioni 3.5 kwa ajili ya upatikanaji wa maji salama na umeme majumbani duniani ifikapo 2030, ikifikisha jumla ya trilioni 97.

“Ripoti hii ya GIH  ambayo inaweza   kupatikana mtandaoni, pia inaelezea kwamba dola trilioni 18, kama asilimia 19 ya dola trilioni 97, zinaweza kukosekana iwapo mwenendo wa matumizi ya sasa utaendelea.

“Kila mwaka dola za Marekani trilioni 3.7 zitahitajika kuwekezwa kwenye miundombinu ili kutimiza mahitaji ya uongezekaji wa kasi wa idadi ya watu ulimwenguni, sawa na jumla ya pato la kitaifa la Ujerumani, nchi yenye uchumi wa nne mkubwa duniani,” ilieleza ripoti hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles