22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

Tanzania yaendelea kung’ara kwenye Utalii Bara la Afrika

*UNWTO yaitangaza Tanzania mara ya tatu mfululizo 

Na Mwandishi Wetu, Windhoek- Namibia

Tanzania imeendelea kung’ara ndani ya Bara la Afrika kwa kutangaza vyema vivutio vyake vya Utalii ambapo imeweza kuwa miongoni mwa nchi10 bora kwa mwaka wa tatu mfululizo, kuanzia 2017 hadi 2020.

Ripoti hiyo imetolewa mapema jana 14 Juni kwenye mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Utalii  Duniani  (UNWTO), kupitia kwa Mtaalamu wa utangazaji wa Utalii, Bi. Olga Nowak aliitangaza Tanzania kushika nafasi ya Saba ambayo inakuwa ni mara ya tatu.

Katika mkutano huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro akiwa anaongoza Ujumbe kutoka Tanzania amesema Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi na vya kipekee ambavyo havipatikani mahali popote duniani isipokuwa Tanzania.

Katika kumi bora hiyo, Afrika ya Kusini imetajwa kushika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na nchi ya Misri katika utangazaji vyema ya vivutio vyake vya utalii.

Aidha katika ripoti hiyo, Tanzania imetajwa uendelea kuongoza na kufanya vizuri katika sekta ya utalii licha ya uwepo wa changamoto wa ugonjwa wa UVIKO19 ambao umeikumba karibu Mataifa mbalimbali duniani kote.

Tanzania imekuwa na vivutio mbalimbali vinavyotamba Duniani ikiwemo mlima mrefu barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, Hifadhi zenye vivutio vikubwa vya Wanyama kama Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi ya Nyerere, Hifadhi ya Ruaha, Tarangile,l pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

Katika hatua nyingine Tanzania kushiriki katika mkutano huo wa siku tatu, kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Ndumbaro na ujumbe wak , imepata fursa ya kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hususani viongozi wa Serikali na wadau wa utalii kutoka nchi wanachama wa UNWTO katika kukabiliana na athari za COVID-19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali kwa kufanya vikao vya ana kwa ana na viongozi wanaoshiriki mkutano huo.

Aidha,Tanzania imepata  fursa ya kutoa maoni yake kwa lengo la kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee katika Bara la Afrika ambapo Waziri Dk. Ndumbaro amemkaribisha Mtaalamu wa masuala ya utangazaji kuja Tanzania kutoa ujuzi huo.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara, Bi. Beatrice Kessy  kutoka Hifadhi za Taifa (TANAPA)  ambaye yupo kwenye mkutano huo, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee Barani Afrika ambapo ameomba ushirikiano wa makampuni makubwa ya Kimataifa kuisaidia Tanzania  kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania ili viweze kujulikana na watu wengi duniani.

Ameongeza kuwa, ili kuongeza idadi ya watalii wataokatembelea Tanzania, Makampuni makubwa yanapaswa kuchangamkia fursa ya  kutembelea Tanzania ilikuweza kutangaza vivutio hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles