26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yadorora kwenye ubunifu uilimwenguni

Waziri wa Viwanda, biashara na uwekezaji, Charles Mwijage.
Waziri wa Viwanda, biashara na uwekezaji, Charles Mwijage.

Na Joseph Lino,

The World Intellectual Property Organization (WIPO) imeiweka Tanzania katika nafasi ya 105 dunia katika ubunifu (innovation achievers) kwa mujibu wa ripoti ya  Global Innovation Index (GII) 2016

Afrika Mashariki, Kenya inaongoza katika ubunifu katika nafasi 80, ikifuatia Rwanda (83) Uganda (99) na Burundi ikishika nafasi ya 123. Ripioti hiyo ina chafua na kurudisha nyuma juhudi za Rais John Magufuli za kufanya nchi hii iwe ya  Viwanda kwani ubunifu ni suala muhimu sana  kwenye sekta hiyo.

Ripoti ya GII huchapishwa kila mwaka, lakini ya mwaka huu inaonyesha nafasi za nchi mbalimbali katika mambo ya kiuchumi katika mazingira ya kuwezesha ubunifu ikiwa Tanzania kushika mkia mbele ya Burundi  na  kukaa kwenye nafasi ya 105 kati ya nchi 128 ulimwenguni..

Mauritius inaongoza katika nchi kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kwenye nafasi ya 53, ikifuatia Afrika Kusini (54), Kenya (80), na Rwanda (83), kiwa nchi za jirani kufanya vizuri kuliko Tanzania kama Msumbiji (84), Malawi (98) na Zambia (118).

Ripoti ya GII 2016 inayoitwa Winning with Global Innovation iliandaliwa na ushirikiano Chuo Kikuu cha Cornel na WIPO ilitolewa wiki iliyopita.

“Mwaka huu uchumi wa nchi sita kutoka kusini mwa jangwa la Sahara, Msumbiji, Rwanda, Malawi, Kenya, Uganda na Madagascar ni asilimia 40 wa wabunifu waulimwengu, walifanya vizuri kulinganisha maendeleo ya nchi hizo,” inasema ripoti.

Wastani wa utendaji wa nchi kikanda unaonyesha uwezo katika urahisi wa kuanzisha biashara, Tehama, ubunifu wa mfumo wa biashara, na matumizi katika elimu, pamoja na udhaifu katika makampuni kuendesha tafiti na maendeleo ya kimataifa, mauzo ya nje tekinolojia, ubora wa vyuo vikuu wa ndani na idadi ya machapisho ya kisayansi.

Kupungua kwa ukuaji wa uchumi katika  nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara,  GII 2016 inaonyesha kwamba nchi hizi  lazima zihifadhi ubunifu wake sasa, wakati zinaendelea kuwekeza katika  uzalishaji wa mafuta na mapato yanatokana na  bidhaa

Taarifa za GII 2016 inafafanua pia maendeleo ya dunia yaliongezeka kwa asilimia nne mwaka 2014 kutokana kupungua kwa ukuaji  wa maendeleo kwa nchi nyingi.

“Uwekezaji katika ubunifu ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa muda mrefu, hali ya sasa ya kiuchumi, inahitaji vyanzo vipya vya uchumi na fursa ya mikopo ya mtaji zilizotolewa kwaajili ya ubunifu wa kimataifa ni vipaumbele kwa wadau wote.”  anasema Mkurugenzi Mkuu wa WIPO, Francis Gurry.

“Uchumi unahitaji kuzingatia kuleta mageuzi ya elimu na kuongezeka kwa uwezo wa utafiti kushindana kwa ufanisi katika ulimwengu  ambao haraka hubadilishwa  na utandawazi. ” anasema mhadhiri wa chuo cha biashara Cornell, Soumitra Dutta.

Nchi ambazo zinaongoza dunia katika ubunifu na uvumbuzi, ni  Uswisi, Sweden, Uingereza, Marekani, Finland  na Singapore.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles