24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yachaguliwa kuendesha kampeni ‘Linda Ardhi ya Mwanamke’

Asha Bani, Dar es Salaam

Tanzania imechaguliwa kuwa nchi ya kwanza kuendesha kampeni ya ‘Linda Ardhi ya Mwanamke’ itakayomsaidia mwanamke kuweza kumiliki ardhi yake mwenyewe.

Kampeni hiyo itazinduliwa kesho na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu itakayofanyika katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatano Novemba 20, Mwenyekiti wa kampeni hiyo, Tike Mwambipile kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) amesema kampeni hiyo itajumuisha taasisi 26 ambazo zimelenga kuhakikisha wanawake wanamiliki ardhi.

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kufunga ombwe lililopo kati ya sera au sheria na taratibu  za maisha ya kila siku ya jamii za watanzania ikiwamo kubadili fikra za wanajamii kutoka katika mila kandamizi zinazozuia mwanamke kumiliki ardhi.

“Pia kampeni hii italenga kuongeza nguvu ya haki ya wanawake kumiliki ardhi, kutoa maamuzi kuhusu ardhi na kufaidi mapato yatokanayo na ardhi.

“Tanzania imejikita katika malengo manne ambayo ni pamoja na kuondoa mila na desturi kandamizi zinazo wakwamisha wanawake katika kupata haki zao katika ardhi,” amesema Tike.

Pamoja n amambo mengine, amesema pia nchi imejikita katika kuwawezesha wanawake katika kutumia ardhi zao kwa manufaa hasa ya kiuchumi ,kuongeza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya kutoa maamuzi.

“Kampeni hii ina malengo endelevu ikiwa ni pamoja na kuwezesha wanawake kumiliki na kufaidi mapato yatokanayo na ardhi inayoenda sambamba na malengo namba moja ya kutokomeza umaskini, kukomesha njaa na usawa wa jinsia,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles