31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania ya viwanda inavyohitaji mazingira bora kukuza ubunifu wa kiteknolojia

Na mwandishi wetu

DAR ES SALAAM: Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia mkoani Mbeya, wiki iliyopita kilifanya maonyesho ya kiteknolojia na kuwakutanisha wanafunzi, waalimu wa vyuo na wataalam wa taasisi mbalimbali katika mkoa huo na jadili fursa mbalimbali zitokanazo na ubunifu wa kiteknolojia.

Mkuu wa Kitivo cha Sayansi na Elimu ya Ufundi chuoni hapo Dakta John John katika hotoba yake aliiomba na kuisihi Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini (COSTECH) kutengeneza mfuko wa fedha kutambua na kusaidia vyuo na wanafunzi katika tafiti na maendeleo.

Dakta John alisema mfuko huo wa utasaidia namna ya kukuza ubunifu wa kibiashara, teknolojia na utanufaisha taifa katika lengo lake la kuwa na uchumi wa viwanda jambo ambalo sote tunafahamu ni lengo la Rais Dakta John Pombe Magufuli katika hii awamu ya tano.

Alisema Kutokana na ukweli huo ni vema tukajadili na kutafakari namna gani kama taifa tunaweza kuwa na mipango inayokuza ubunifu katika teknolojia na kuwawekea vijana mazingira mazuri ya kukuza ubunifu ili kusukuma mbele kasi ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Aliongeza kuwa hatuhitaji kutazama mbali kuona matunda ya uchumi bunifu katika zama hizi za teknolojia, alitoa mfano sekta ya mawasiliano ya simu namna ambavyo imekua si tu kwa ajili ya kupiga ama kupokea simu na kutuma meseji bali simu sasa inatuma fedha, inaperuzi mtandao ‘interneti’, inatusaidia kupata huduma za afya na vitu vingine vingi ambavyo ni msaada kwa jamii.

Dokta John alizitaka sekta zingine kuiga mfano katika sekta ya mawasiliano ya simu na kujifunza kuhusu ubunifu na kuweka mazingira bora ya biashara.

Aliongeza kuwa, kwa bahati nzuri sera ya kujenga mazingira bora na endelevu ya biashara imo katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa serikali na kwamba ikifuatwa vizuri itakuwa ni msingi wa kujenga ubunifu wa kiteknolojia ambao leo tunauona na kufaidika na matunda yake katika sekta ya mawasiliano ya simu. .

Alimalizia kwa kusema ubunifu katika teknolojia tunauhitaji ili kujenga Tanzania ya viwanda kama ambavyo tumeuona kwenye sekta ya mawasiliano ya simu utawezekana kama tukiendelea kujenga mazingira rafiki ya kufanya biashara na kuunga mkono uwekezaji toka sekta binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles