24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

TANZANIA YA PILI EAC KIWANGO KIDOGO CHA RUSHWA

BERLIN, UJERUMANI


TANZANIA imepanda kutoka nafasi ya 116 ya orodha ya viwango vya rushwa duniani hadi 103 na hivyo kushika nafasi ya pili kwa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa na kiwango cha chini cha rushwa baada ya Rwanda.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya 2017 iliyochapishwa juzi na Shirika la kimataifa la kukabiliana na rushwa la Transparent International (TI), ambayo imehusisha nchi 180 duniani.

Alama zinazotokana na takwimu za mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo Afrika na Jukwaa la Uchumi la Dunia, zimehesabiwa kati ya 0 na 100; kiwango cha juu zaidi cha rushwa kikiwa 0 na 100 kiwango kidogo.

Tanzania ilipata alama 36 kati ya 100 huku Rwanda, ambayo imekuwa ikiongoza kwa miaka mingi sasa kwa kiwango kidogo cha rushwa ukanda huu, ikipata alama 55 na kushika nafasi ya 48 duniani.

Kenya ilikuwa ya tatu kwa kupata alama 28 na kushika nafasi ya 143 duniani ikifuatiwa na Uganda alama 26 nafasi ya 151 na Burundi alama 22 nafasi ya 157.

Wakati Uganda licha ya kupata nyongeza ya alama moja imeshika nafasi ile ile ya mwaka uliopita, Tanzania ilipata nyongeza ya alama nne zaidi zilizoipandisha nafasi 13.

Rwanda ilipanda kwa nafasi tano baada ya kupata ziada ya alama tano kulinganisha na mwaka uliopita, ikifuatiwa na Kenya nafasi mbili kwa ziada ya alama mbili ilizopata 2016.

Sudan Kusini na Somalia ndizo nchi zinazonuka rushwa zaidi duniani zikishika nafasi mbili za mkiani; 179 na 180 kwa kupata alama 12 na 9.

Nchi 12 zilizoshika nafasi za juu kwa kiwango kidogo cha rushwa duniani na alama zao katika mabano ni New Zealand (89), Denmark (88), Finland, Norway na Uswisi (85), Singapore na Sweden (84), Canada, Luxembourg, Uholanzi na Uingereza (82) na Ujerumani (81).

Miongoni mwa nchi zilizo na kiwango cha kati cha rushwa ni Marekani na Ubelgiji zilizopata alama 75, zikifuatiwa na Japan (73), Ufaransa (70), Hispania (57) na Italia (50).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles