27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Tanzania wenyeji shindano la warembo viziwi Afrika

JEREMIA ERNEST

Shindano la urembo la viziwi Afrika ‘Miss na Mister Deaf Afrika’ linatarajiwa kufanyika hapa nchini Aprili 2020.

Mchuano huo utahusisha nchi za Afrika na kila nchi itatoa washiriki wa wiki ambapo mshindi ataiwakilisha Afrika katika mashindano ya dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari kiongozi wa viziwi, Habibu Mlope amesema hii ni nafasi ya upendeleo kwa nchi hivyo wadau na serekali wajitokeze kuunga mkono ugeni huo.

“Tumepata nafasi ya kuwa wenyeji wa mashindano haya mwaka huu tunaomba wadau na serekali kuwa pamoja na sisi katika maandalizi ili kuijengea heshima nchi yetu kwa kuthamini watu wenye ulemavu kama sisi,” amesema Habibu.

Ameongeza kuwa kabla ya mchuano huo kutakua na shindano la ndani ili kupata wawakilishi watakaoiwakilisha nchi katika shindano la Afrika.

Aidha ameishukuru serekali ya awamua ya tano kwa kuunga mkono mashindano haya ya urembo hapa nchini na kuwapa kipau mbele kama ilivyo mashindano mengine.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles