25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TANZANIA QUEENS KUIVAA NIGERIA LEO

Na MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘Tanzanite Queens’, leo inatarajia kushuka dimbani kuwakabili wenyeji wao, Nigeria, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Ufaransa Desemba, mwaka huu.

Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Samuel Ogbemudia, ulioko Jiji la Benin, kabla ya timu hizo kurudiana wiki mbili baadaye nchini Tanzania, ambapo mshindi wa jumla wa michezo hiyo atacheza mechi nyingine mbili dhidi ya Morocco, kabla ya kufuzu kwa fainali hizo.

Kikosi cha Tanzanite Queens kiliondoka nchini usiku wa kuamkia Alhamisi kikiwa na wachezaji 20, watu 11 kutoka benchi la ufundi pamoja na viongozi watatu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Timu hiyo haina uzoefu wa kutosha katika mechi za mashindano, kutokana na kuundwa hivi karibuni na wachezaji ambao wanatoka kwenye shule mbalimbali hapa nchini.

Licha ya kutopata michezo ya kimataifa ya kirafiki kabla ya kuvaana na Nigeria, kocha wa kikosi hicho, Sebastian Nkoma, alisema amewaandaa vizuri kisaikolojia kwa ajili ya kupambana bila kujali kuwa watakuwa ugenini.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huo, japo hatukupata michezo ya kirafiki tuliyoitaka, hatujavunjika moyo na tunakwenda kupambana ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo huo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles