Na Jeremia Ernesta, Mtanzania Digital
Klabu ya Tanzania Prisons inayoshiriki Ligi Kuu soka Tanzania Bara, imepata udhamini kutoka kampuni ya Sokabet inayo endesha michezo ya kubahatisha nchini.
Klabu hiyo ambayo imemaliza msimu huu kwa kushika nafasi ya saba kati 18 za ligi kuu 2020-2021.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 19, 2021 Msemaji wa Sokabet ambaye pia ni Meneja Oparesheni, Ahmet Akmar Men, amesema mkataba wao na Tanzania Prisons umejikita katika kuhakikisha timu inakuwa na hali nzuri kuanzia kwenye usajili, uendeshaji, maradhi pia kufanya kazi pamoja na timu zaidi.
“Leo tumesaini mkataba wa kuwa wadhamini wa kuu wa timu ya Tanzania Prisons kwa msimu wa 2021-2022 katika ligi kuu ya Tanzania Bara, kutokana na udhamini wetu timu hii itafanya uboreshaji wa kiwango cha juu katika kikosi chake ili kufikia malengo ya kufanya vizuri katika msimu ambao dirisha
la usajili limefunguliwa leo,” amesema.
Kwa upande wa Tanzania Prisons Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Mkwanda Mkwanda, amesema wamefurahi kuingia mkataba na kampuni ya Sokabet.
“Tunazo changamoto nyingi kama ukosefu wa vifaa, viwanja vya mazoezi na nyingine, hivyo tutatumia hii nafasi kama fursa na kuhakikisha tunafanya vizuri ili kuendeleza soka letu, pia tuna waalika na makampuni mengine kuja kuweza timu yetu,” amesema Mkwanda.
Ameongeza kuwa suala la mpira wa miguu ni jambo lenye kushika maslahi ya watu wengi, hivyo kuingia mkataba na kampuni ya Sokabet ni imani yetu tutafanya vizuri.
“Tutatumia hii nafasi kama fursa na kuhakikisha tunafanya vizuri ili kuendeleza soka letu, pia tuna waalika na makampuni mengine kuja kuweza katika timu yetu,” amesema .