26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania Prisons yajitosa rasmi soka la wanawake

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

UONGOZI wa Klabu ya Tanzania Prisons umetangaza kuanzisha timu ya soka ya wanawake inayoitwa Tanzania Prisons Queens, huku wakitamba kuja kuleta ushindani katika mchezo huo.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Oktoba 2, 2023, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Ajabu Kifukwe, amesema tayari wana jumla ya wachezaji 23 na wanatarajia kuongeza wengine, lengo likiwa kutengeneza kikosi imara cha ushindani.

Kifukwe amebainisha kuwa timu hiyo ya awali waliyounda itaanza kushiriki Ligi ya Mkoa lakini baadaye Ligi Kuu ya Wanawake na mashindano mengine.

“Tumeamua kuanzisha timu ya wanawake baada ya kuona umuhimu wa kufanya hiyo kwa sababu uwezo tunao na tuna kila kitu cha kuweza kuendesha timu hiyo. Pia utaratibu uliopo sasa kila klabu inatakiwa kuwa na timu ya wanawake.

“Tumefikiria tukaona ni aibu klabu kubwa kama Tanzania Prisons kukosa timu ya wanawake, tutaanzia nchini lakini lengo letu ni kuwa na timu Ligi Kuu ya Wanawake. Tuantarajia kuweka wazi mikakati yetu hivi karibu kila mmoja kufahamu tulivyojipanga,” ameeleza Kifukwe.

Amesema timu hiyo makao makuu yake yatakuwa Chuo cha Ufundi cha Magereza Ruanda kilichopo jijini Mbeya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles