31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania na Italia kuongeza nguvu sekta ya Bishara na Uwekezaji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Tanzania na Italia zimeahidi kushirikiana kukuza na kuendeleza sekta ya biashara ya uwekezaji kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Akihutubia Juni 3, katika sherehe za Maadhimisho ya 76 ya siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya Italia iliyofanyika Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema Tanzania imeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kuwasihi wafanyabiashara wa Italia kuja kuwekeza nchini kwa kuwa ni salama zaidi.

Balozi wa Italia nchini, Marco Lombardi, akizungumza kwenye hafla hiyo.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa, Tanzania na Italia zimekuwa na utamaduni wa kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kupitia majukwaa mbalimbali ya biashara na matokeo chanya ya majukwaa hayo yameanza kuonekana ambapo Desemba, 2021 kupitia kongamano la biashara na uwekezaji lililofanyika Italia.

Kampuni ya Kiitaliano ya ‘Suness Limited’ inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ilisaini makubaliano na Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kwa ajili ya kuendeleza mradi wa shaba inayopatikana Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Balozi wa Italia nchini, Marco Lombardi ameipongeza Tanzania kwa jitihada kubwa za kuboresha na kuimarisha mazingira ya biashara nchini.

Ameongeza kuwa kuwa kitendo cha Tanzania kuviondoa vikwazo vya biashara kimeongeza imani kubwa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wengi duniani kuiona Tanzania ni salama.

Aidha, Balozi Lombard amempongeza Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuimarisha Diplomasia ya Uchumi na mataifa mengine duniani.

Tanzania na Italia zimekuwa zikishirikiana katika Nyanja za kilimo, afya, elimu, maji, nishati, utalii na maendeleo ya sekta binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles