31.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 19, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Tanzania kuwa mwenyeji mkutano mkuu wa 19 wa wadau wa Korosho Afrika (ACA)

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kwa siku mbili mfululizo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa 19 wa Shirikisho la Wadau wa Korosho Afrika (ACA) utakaofanyika Novemba 18 na 19, 2025 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julias Nyerere

Mkutano huo unafanyika sambamba na maonyesho ya bidhaa na teknolojia za kuzalisha na kusindika zao hilo, utawakutanisha wadau tofauti waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa zao hilo kutoka ndani na je ya Afrika.

Akizungumza Dar es Salaam leo Januari 31, 2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred, amesema mkutano huu unatarajiwa kuwakutanisha zaidi ya washiriki 500 kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na wawakilishi kutoka nchi 30 barani Afrika.

Amesema pamoja na mambo mengine, lengo la mkutano huu ni kufungua fursa za uwekezaji kwenye tasnia ya korosho huku kauli mbiu ikiwa “Korosho kwa Ukuaji wa Uchumi Endelevu”. 

“Mkutano huu ni jukwaa muhimu kwa wadau wa sekta ya kilimo cha korosho kujadili changamoto, fursa za uwekezaji, na njia bora za kuboresha sekta hiyo. Serikali ya Tanzania imeweka mikakati madhubuti ya kuboresha sekta ya korosho ili kuongeza uzalishaji na kuchochea ajira kwa vijana,” amesema Alfred.

Upande wake Mkurugenzi wa Jukwaa la Korosho Afrika (ACA), Ernest Mintah , mkutano huu ni fursa kwa Tanzania kujifunza kutoka kwa nchi zilizoendelea katika sekta ya korosho, kama vile Ivory Coast, ambayo imepiga hatua kubwa katika uzalishaji na usindikaji wa korosho. 

“Mkutano wa 19 wa Korosho Afrika utakuwa jukwaa muhimu kwa wakulima, wawekezaji, na wadau wa sekta ya kilimo cha korosho kujadili mbinu bora za kuimarisha sekta hii.  Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa korosho duniani, mkutano huu ni fursa adhimu ya kuhakikisha sekta hii inakua na kuchangia zaidi uchumi wa nchi,” amesema Mintah.

Ameogeza kuwa takwimu zinaonyesha Afrika inazo zaidi ya hekta 600,000 za ardhi safi inayofaa kwa kilimo lakini hazitumiki hivyo ni uwekezaji pekee utakaowashawishi vijana kuchangamkia fursa zilizopo kwenye kilimo na kuzitumia hekta hizo kwa manufaa.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wabanguaji wa Korosho Tanzania (TACP), Bahati Mayoma, amesema kuwa mkutano huu utaleta mjadala wa kina kuhusu masuala ya uzalishaji, ubanguaji, rasilimali watu, na soko la kimataifa la korosho.

Tanzania inazalisha korosho bora zaidi duniani ikiwa ya nne Afrika ikitumia wastani wa hekta 300,000 sawa na asilimia mbili ya eneo zima ililonalo lakini, amesema kiasi kikubwa kinasafirishwa nje ya nje na kwenda kutoa ajira huko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
594,000SubscribersSubscribe

Latest Articles