29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Tanzania kutumia fursa za uwekezaji kutoka Benki ya Afrexi

*Kupata fursa lukuki, dira ya Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Lameck Nchemba amemuahidi Rais wa Benki ya Afrexim kuongeza mtaji wa ziada katika Benki hiyo ambayo Tanzania inamiliki hisa ili iwe na wigo mpana wa kuendelea kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) na Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah (hayupo pichani), jijini Dodoma.

Dk. Nchemba ametoa ahadi hiyo Julai 19, 2022 jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah, ambapo walijadili masuala kadhaa likiwemo fursa zinazotolewa na Benki hiyo.

Dk. Nchemba alisema kuwa Serikali itashirikiana na Benki hiyo ambayo kuanzishwa kwake kulikuwa na lengo la kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika nchi za Afrika.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

“Tunatekeleza dira ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ya kuweza kuvutia uwekezaji, kuendeleza maeneo mahususi ya uwekezaji (EPZ) pamoja na upande wa Zanzibar ambayo inakusudiwa kutengeneza ajira nyingi kwa vijana ili pato la mtanzania mmojammoja liongezeke na kuweza kupunguza umasikini,” alieleza Dk. Nchemba.

Aidha, Dk. Nchemba amesema kuwa Tanzania inaahidi kuendelea kufanyakazi pamoja na ofisi ya Rais huyo kwa kuzishirikisha Wizara zake, ikiwemo ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Wizara ya Kilimo na Afya ili kuweza kutumia fursa zilizobainishwa na Benki hiyo.

Kwa upande wake Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah, alisema kuwa Benki yake inafursa nyingi zikiwemo za mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya na viwanda.

Alizitaja fursa nyingine ambazo Tanzania inaweza kuzipata kuwa ni pamoja na kuwezesha Kanda maalum za kiuchumi, kuongeza thamani ya mazao ya kilimo pamoja na uwekezaji katika hisa kupitia taasisi za fedha.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa sita kushoto) na Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah (wa tano kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Tanzania na Benki ya Afrexim, jijini Dodoma.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles