Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital
Shirika la REPSSI linatarajia kufanya kongamano lake la sita linalofahamika kama Msaada wa Kisaikojia na Kijamii lenye kauli mbiu ya buni, jumhisha na stawi ukiwa ni mwendelezo wake wa kuandaa makongamo hayo kwenye nchi mbalimbali kila baada ya miaka miwili.
Kwa mwaka huu kongamano hilo linatarajiwa kufanyika nchini Msumbiji kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo kupitia Wizara ya Watoto kwa njia ya mtandao kutokana na changamoto ya janga la virusi vya corona ambalo limeleta shida kubwa kwa jamii nyingi.
Akizungumza leo Jumatano Agosti 18, kwenye mkuno wa kuelekea kongamano hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa REPSSI, Patrick Mangen, amesema msaada wa kisaikolojia ndio kitu kikubwa kinachohitajika ili kuondoa taharuki ya corona katika jamii zetu.
“Kama tunavyofahamu kwamba kwa mwaka huu janga la corona limeweza kutuyumbisha huku likileta changamoto kadhaa kwenye jamii zetu wakiwamo watoto kupata mimba na ndoa za utotoni, hata hivyo tunaona kwamba pamoja na mambo mengi kufanywa na kuandikwa juu ya mlipuko huu lakini msaada wa kisaikolojia ndio unaohitajika zaidi ili kuondoa changamoto hizi zinazoikabili jamii zetu.
“Hivyo katika kongamano la mwaka huu litakalofanyika kwa njia ya mtandao kuanzia Oktoba 13 hadi 15, tutakuwa na washika dau muhimu wakiwamo watunga sera, serikali, wanasaikolojia na watu wengine muhimu, kutokana na changamoto ya corona.
“Hivyo kupitia mkutano huo tutatoka na maazimio mapya, ikiwamo kubuni vitu vipya vitakavyozisaidia jamii zetu zilizoko kwenye ukanda ambao Repssi inafanyakazi,” amesema Mangen.
Mangen ameongeza kuwa kongamano hilo litajikita zaidi kuangalia namna ya kukabiliana na kuondoa taharuki katika jamii katika changamoto mbalimbali ukiacha ya corona.
“Hivyo tunatajia kuja na mawazo bunifu yeney kujenga kupitia kongamano hili ili kuwa na jamii yenye ustawi bora katika maeneo mbalimbali, kwani ni kujumu letu kujenga jamii yenye ustawi bora,” amesema Mangen.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa REPSSI Tanzania, Edwick Mapalala, amesema kwa Tanzania, Mikoa ya Kagera na Dar es Salaam kutakuwa ni vituo vya kongamano hilo.
Amesema lengo kuu hasa ni kujadili umuhimu wa msaada wa kisaikolojia hasa kwa watoto nyakati za majanga, ikiwemo corona, na kwamba janga hilo linavyoendelea ndipo kisaikolojia pia mtu anaathirika.
Mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni ni kati ya mambo yatakayo jadiliwa..
Kongamano hilo la sita ambalo linajumhisha nchi 13 za Angola, Botswana, Msumbji, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Namibia, Uganda, Kenya, Lesotho, Tanzaania, Afrika Kusini na Eswatini linafadhiriwa na na Serikali ya Sweeden.