30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

Tanzania kuendeleza kilimo umwagiliaji  mkubwa

Na Mwandishi WetuRASILIMALI  Maji ni ya mzunguko na kama itawekwa vizuri matumizi yake katika kila hatua huleta manufaa makubwa kwa kilimo  kupitia umwagiliaji  na kupata nishati ya umeme kwenye maporomoko.

Mzunguko wa maji, pia unaitwa mzunguko wa hydrologic yaani mzunguko unaohusisha mzunguko unaoendelea wa maji katika mfumo wa dunia-anga. Kati ya michakato mingi inayohusika katika mzunguko wa maji, muhimu zaidi ni  kugeuza maji kuwa hewa (evaporation), kupumua kwa kuwa maji tena ( condensation and  precipitation)  na mtiririkowake kwenye vijito, mito na maziwa (runoff).

Rasilimali  Maji hutoka kwenye hifadhi moja hadi nyingine, kama vile kutoka mto hadi baharini, au kutoka baharini mpaka anga, na michakato ya kimwili ya uvukizi, (condensation, precipitation, infiltration, runoff) na mtiririko subsurface. Kwa kufanya hivyo, maji huenda kwa njia mbalimbali: kioevu, imara (barafu) na mvuke na kurudia tena.

Kauli kuwa kilimo ni maji inajipambanua zaidi kwa mpango kabambe wa Tanzania  wa kufanya kilimo cha umwagiliaji maji  kuwa kipaumbele  kikuu katika mpango wa pili wa Maendeleo Kilimo Mkakati  yaani ASDP II.

Malengo ya kilimo hicho ni kuwezesha ufanyaji wa kilimo biashara , Kilimo samaki  na uvuvi na kilimo kwenye maeneo kame kutokana na mabadiliko ya hali ya nchi.

Tanzania jna mabonde tisa (basins) na juhudi za kilimo zimeelekezwa huko kwenye Mabonde ili kumwagilia maji.

Kwenye matumizi ya maji sadifu na kwa gharama nafuu ni mifano ya kule India na Misri ambao wanalima kwenye mabonde yote na jangwani na la maana zaidi ni kuwa India maji yake hutumika mara 6 kabla ya kuishia baharini. Tanzania mito yetu mingi hupeleka maji yake baharini  bila kuwa na matumizi rejea na hivyo  kuonekana kuna uhaba wa maji na tathimini iloyofanyika imeonesha kuwa asilimia tano tu ya kilimo cake kiko kwenye umwagiliaji maji huku nchini imebaraikiwa kwa maji ya maziwa makuu matatu na mito mingi kama michirizi ya damu.

Miradi ya umwagiliaji

Tanzania sasa imejipanga sawa katika suala zima la kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza tija ya kuongeza kiasi cha mazao yatakayozalishwa kwa uwingi na ubora wake na hivyo kutoa faida kubwa na kuoondoa umaskini usio wa lazima nchini kwani ardhi ya kufanya kilimo ipo yakutosha.

Kuzingatia dhamira hiyo serikali imetenga kiasi cha shilingi trilioni 2.2 kwenye mfuko  utakaoanza kutoa fedha mwaka huu kwa hitaji hilo ili kuboresha  mipango ya umwagiliaji nchini Bunge liliambiwa na Naibu Waziri wa Maji Omari Mgumba zikiwa ni sehemu ya fedha kiasi cha shilingi Trilioni 13 za ASDP II.

Mpango huo Utaongeza kilimo kutoka hekta 460,000 mwanzo wa mradi hadi kufiki hekta Milioni  Moja mwishoni mwa mradi mwaka 2020.

Akielezea Mpango huo alisema sasa unafanyiwa tathimini yakinifu  katika mabonde mbalimbali ili  kupata picha kamili ya tatizo lenyewe na namna ya kuboresha ili kuweza kufanya kilimo cha umwagiliaji maji.

Mgumba alikuwa akimjibu Mbunge wa Viti Malumu wa Chadema, Yosepheter Komba aliyetaka kujua mipango ya serikali ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji maji nchini.

Alisema serikali imefanya mapitio ya mradi wa mwaka 2002 na kuainisha maeneo ya kipaumbele ambayo yatashugulikiwa katika awamu mbili za kati ya  2018/19  na  2025/26  ya miaka ya fedha husika.

Hali iliyopo sasa ni kuwa asilimia Tano tu ya hekta 29.5 milioni  ya ardhi inayoweza kufanyiwa umwagiliaji inatumika hivyo.

Wataalamu wa kilimo wanasema kuwa  kutokana na hali ya ukame utokanao  na mabadiliko ya hali ya nchi inaathiri  kilimo kinachotegemea mvua  na mafuriko kuwa haba  kwa mazao kama ya mpunga na hivyo uchumi  kuumia kwa kupungua uzalishaji na vivyo kwa wakulima wadogo kukosa usalama wa chakula na hivyo kufanya umwagiliaji  maji kuwa kipaumbele ili kunusuru mdororo wa uchumi na chakula.

Hivi basi juhudi za serikali katika kuinua kilimo cha chakula na mazao ya baishara zimekumbwa na sintofahamu itokanayo kwa kukosekana kwa mifumo sahihi na miundombinu stahiki ya umwagiliaji maji pamoja na uendelezaji na utunzaji wake.

Kilimo ni maji na kukosekana kwake mara nyingi huwa ni janga kubwa kwake.

Hivi basi wataalamu wanadai inatakiwa mipango  tangamano na inayoingiliana ya umwagiliaji maji na kuifanya kuwa iwe endelevu kwa kujali na kutambua wajibu wa wakulima na changamoto zao katika kuendeleza sekta hiyo.

Hatua za serikali

Kwa upande wake serikali imelivalia njuga suala hilo kwa kufanya matayarisho  na marekebisho  ya mifumo na mwenendo wa utendaji kazi ili kuimarisha suala zima la kilimo cha umwagiliaji.

Serikali imechukua  hatua  sadifu za kuimarisha muundo wake  na utendaji kazi kwa Wizara ya Maji kukabidhi Tume ya Umwagiliaji kwa Wizara ya Kilimo na pamoja nayo wizara imekabidhi pia mpango kabambe wa umwagiliaji unaoainisha maeneo ya kilimo na maji yalipo.

Mpango huo unalenga angalau kumwagilia hekta zipatazo milioni moja za kilimo nchini.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo alisema mpango huo umesainiwa Julai mwaka huu kwa ajili ya matumizi na ni nyenzo muhimu ya kufanikisha kukua sekta hiyo ya umwagiliaji  nchini.

“Mpango huo ni mpya na umeidhinishwa kwa ajili ya kukuza sekta ya umwagiliaji. Wizara ya Maji tumebaki na jukumu  la kukupa maji,” alisema.

Profesa Mkumbo  alisema ili kuongeza ufanisi katika umwagiliaji katika kilimo kama sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II), serikali imeamua kuhamishia umwagiliaji kwenye wizara hiyo.

“Uamuzi huu unalenga kuiwezesha wizara yenye dhamana ya sekta ya maji kudhibiti matumizi ya maji katika umwagiliaji bila kuwa na mgongano wa kimajukumu,” alisema.

Alisema sekta ya umwagiliaji ndiyo inayoongoza kwa matumizi ya maji nchini ambapo kiwango cha matumizi ya maji kwa umwagiliaji kinakadiriwa kuwa mita za ujazo milioni 10,309 kwa mwaka.

“Matumizi ya maji kwa umwagiliaji ni sawa na asilimia 83.6 ya matumizi ya maji yote nchini, hivyo Tume hii itawajibika kiutawala kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na jina la Wizara ya Maji na Umwagiliaji litabadilika na kubaki kuwa Wizara ya Maji pekee,” alisema Mkumbo.

Nyaraka nyingine zilizokabidhiwa ni za Sera ya Umwagiliaji na ile Sheria ya Umwagiliaji. Aidha, Profesa Mkumbo alisema utekelezaji wa uhamisho utatekelezwa hatua kwa hatua mwaka mzima hadi marekebisho ya Hati ya Mgawanyo wa majukumu ya wizara hizo utakapokamilika.

“Utendaji wa Tume ya Umwagiliaji utakuwa chini ya Wizara ya Kilimo, lakini kifungu cha fedha kwa bajeti ya mwaka 2018/19 kitaendelea kuwa chini ya Wizara ya Maji,” alisema.

Uwekezaji skimu za umwagiliaji 3000

Wataalamu wa Kilimo na wachumi wanakubaliana na wanadai pasi na shaka kuwa kilimo ni maji na hivyo wanasisitiza kuwa azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati itafikiwa tu ikiwa kutakuwa na mipango madhubuti ya kilimo cha umwagiliaji maji na kwa kuanzia ni kufufua miradi iliyokufa.

 

Kwa kutambua suala hilo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika muendelezo wa majukumu yake imejipanga kufufua skimu za umwagiliaji nchini ili kuwezesha wakulima kuongeza uzalishaji bila kutegemea mvua kama ilivyo sasa.

 

Mkurugenzi wa uendeshaji wa tume hiyo, Anthony Nyarubamba aliwaambia waandishi wa habari mjini Bariadi wakati wa Maonesho ya Nane Nane mwaka huu kuwa mpango huo  wa serikali unalenga kuhakikisha skimu zote 2,964 zilizosajiliwa nchini zinafanya kazi. Hivi sasa ni  skimu 69 pekee zinafanya kazi na hivyo kutafsiriwa kiwango cha ukubwa wa kazi mbele yake. Itakuwa fumua fukua katika mabonde yote makuu 9 ya Tanzania.

 

Nyarubamba alisema mkakati huo utaenda sambamba na usajili wa skimu mpya kwa mujibu wa sheria namba 5 ya mwaka 2013 ya usajili ambayo tayari imefanikisha usajili wa skimu mpya 80.

Alisema akiwa katika viwanja vya Nyakabindi mjini Bariadi, ambako maonesho ya Nanenane kitaifa yalifanyika mwaka huu  chini ya usimamizi wa karibu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka ambaye ana imani kubwa juu ya mapinduzi ya kilimo yatokanayo na kilimo cha umwagiliaji.

 

Alisema Kilimo cha umwagiliaji ndicho chenye uhakika wa mavuno kwa sababu kinamhakikishia mkulima uzalishaji kipindi chote cha mwaka bila kutegemea mvua na hivyo kufanya kilimo hicho kuwa endelevu  na kuleta tija kwani kunakuwa hakuna kikomo cha utendaji kazi kwa misimu yote.

Kuna matatizo mengi katika masuala ya umwagiliaji na mengi yametokana na wakulima wenyewe ambao wanona umwagiliaji ni usumbufu kwa kukosa uelewa wa kina wa suala zima.

 

Ofisa maendeleo ya jamii kutoka idara ya uwezeshaji na uendeshaji wa Tume ya Umwagiliaji, Zukheri Huddi alitaja baadhi ya changamoto zilizokwamisha maendeleo ya skimu za umwagiliaji kuwa, ni wakulima kukosa umakini katika usimamizi na matumizi ya skimu zao na kukosa ushauri wa kitaalamu.

 

Anasema baadhi ya skimu zimeharibika kwa kujaa michanga, majani, kutofanyiwa usafi na mipasuko. Haya ni miongoni mwa mambo yatakayosimamiwa na kudhibitiwa na sheria mpya ambayo itatumika katika kufufua skimu hizo.

 

Mwongozo wa uendeshaji

Suala la matumizi ya muongozo imeshauriwa liingizwe katika sheria ndogondogo za  skimu kwa kuwepo kwa motisha kwa watumiaji wazuri wa mwongozo na Tume kuendelea kutoa  maelekezo kwa wadau mbalimbali ambayo kwa Uwepo na ufuatiliji kwa ngazi zote wa mara kwa mara juu ya matumizi ya mwongozo.

Majukumu ya Tume  ya  Taifa ni kutoa  elimu ya  mwongozo kwa wadau mbalimbali wa umwagiliaji kwa Kusimamia na kuratibu matumizi ya mwongozo ikiwamo Kutoa  maelekezo/maagizo kwa wadau mbalimbali ambayo yatawezesha kila mmoja kutumia muongozo.

 

Ngazi ya Mkoa

Katika ngazi ya mkoa majukumu ni  Kutoa  elimu ya mwongozo kwa wadau mbalimbali wa umwagiliaji na kuratibu na  kusimamia  matumizi ya mwongozo,

Kusambaza (dissemination) mwongozo kwa wadau  na Kuweka mfumo wa utoaji wa motisha kwa watumiaji wazuri wa muongozo huo na Kupokea na kutekeleza  maelekezo/maagizo kwa wadau  ikiwemo Kutoa msaada wa kitaalamu wa usanifu na usimamizi wa ujenzi

Faida ya mwongozo

Mwongozo husaidia kuwepo kwa miundombinu yenye ubora unaotakiwa na itakayodumu kwa muda mrefu,

husaidia  vile vile kuwepo kwa mifumo inayofanana katika sekta ya uendelezaji wa kilimo cha umwagiliaji.

Utumiaji wa mwongozo husaidia skimu za umwagiliaji kuwa endelevu  na hivyo husaidia kuwepo kwa uwajibikaji kwa wadau wote wa umwagiliaji isitoshe Mwongozo husaidia kuongeza tija katika skimu za umwagiliaji maji.

Mwogonzo  nao husaidia kuwepo kwa kumbukumbu /taarifa sahihi kwa ajili ya kuandaa mipango ya baadae.  Pia utumiaji wa mwongozo husaidia kupunguza migogoro miongoni mwa wadau wa umwagiliaji.

 Kilimo cha mpunga

Kilimo cha umwagiliaji  hitaji lake ni a bayana sana kwenye kilimo cha zao la mpunga ambalo linahitaji maji kwa wingi  na hata mafuriko kama itawezekana kirahisi.

Tanzania imeshindwa  kutumia uwepo wa soko la zaidi ya shilingi trilioni moja Afrika ya Mashariki kwani ina uwezo wa kuzalisha asilimia 70 ya mahitaji ya mchele wa eneo hili lakini uzalishaji  bado ni tatizo ingawa sasa inazalisha ziada ya kuweza kuuza nje.

Kwenye mkutano wa Saba wa Wazalishaji wa Nafaka na Biashara (Seventh African Grain Trade Summit) uliokuwa na dhamira ya Uwekaji Malengo Mapya ya  Fikara za Biashara kwa Chakula na Ustawi Afrika (Setting New Horizons Rethinking Grain Trade for Food Security and Prosperity in Africa)  Mwenyekiti wa  Baraza la Mchele Tanzania, Julius Wambura alisema Afrika huagiza toka nje ya bara hili mchele wa thamani ya Dola Bilioni 40 kila mwaka kutoka Asia  wakati kuna zaidi ya asilimia 60 ya ardhi yake inafaa kwa kilimo.

Akizungumzia Afrika Mashariki alisema hutumia Dola Milioni 500 kuagiza mchele wakati Tanzania ina uwezo wa kufikia asilimi 70 ya mahitaji. Hii inatolea wajkati wakulima wake hawana soko la uhakika  kwani nchi nyingine wanachama  hutoa mikwala ya kibiashara kuzuia.

Walipoulizwa mawaziri wa Kilimo  na yule wa Biashara wa wakati huo Mawaziri Dk Tizeba na mwinzie  Mwijage walisema msisitizo ni kujitosheleza nyumbani kwanza.

Taraifa za Food and Agriculture Organisation (FAO) zinaonesha Tanzania mwaka 2011 iliuza mchele  nje tani  76,000.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,702FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles