22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

TANZANIA, KENYA ZASAINI MAKUBALIANO YA KIBIASHARA

Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

Tanzania na Kenya zimesaini makubaliano ya uwekezaji kurahisisha shughuli za kibiashara zinazofanywa katika nchi hizo.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo leo Alhamisi Julai 5, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa Elisante Ole Gabriel amesema, makubaliano hayo yatasaidia kufungua fursa za uwekezaji kwenye biashara na kukuza uchum wan chi hizo mbili.

Amesema kutokana na hali hiyo, Watanzania wanaruhusiwa kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo Kenya na Wakenya wanaruhusiwa kuangalia fursa kama hizo zilizopo Tanzani.

“Tumesaini makubaliano ya kibiashara kati ya Tanzania na Kenya ili kufungua fursa za uwekezaji kwa wafanyabiashara wa nchi hizo mbili, jambo ambalo linaweza kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira,” amesema Profesa Ole Gabriel.

Aidha, amesema hadi mwaka jana, Wakenya waliwekeza kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo zaidi ya 507 kutoka 400 yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani bilioni 1.66, kwa miaka iliyopita, jambo ambalo limechangia kukuza uchumi.

Pamoja na mambo mengine, amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisha wanafungua Kituo Kimoja cha Kibiashara (One Stop Centre) ili kurahisisha shughuli za uwekezaji.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,367FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles