33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘Tanzania ina wagonjwa wa akili 450,000’

christina-mndemeSARAH MOSES Na RAMADHAN HASSAN, DODOMA

TANZANIA ina wagonjwa wa akili 450,000 huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi.

Takwimu hizo zilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme, wakati wa maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani.

Mndeme aliyasema hayo alipokuwa akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Katika hotuba hiyo, Mndeme alisema kutokana na taarifa ya akili ya mwaka 2014/2015, Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa unaongoza kwa kuwa na asilimia mbili ya wagonjwa wa akili ukifuatiwa na Mkoa wa Mwanza wenye asilimia 1.8.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, mkuu huyo wa wilaya alisema mkoa wa mwisho kwa kuwa na idadi ndogo ya wagonjwa hao ni Rukwa wenye asilimia 0.2.

“Ugonjwa wa akili na saikolojia, dalili zake ni pamoja na kubadilika tabia kwa kukataa kula, kukosa usingizi, kujitenga na watu, kutopenda kufanya jambo lolote na kukosa moyo wa kufanya kazi za maendeleo.

“Dalili zingine ni kukosa mtiririko wa mawazo unaoeleweka na kutoeleweka wakati wa kuzungumza, kusikia sauti zisizokuwapo au kuona vitu au watu wasiokuwapo pamoja na mhusika kutojithamini na kutojijali,” alisema Mndeme.

“Wagonjwa wa akili wamekuwa wakibaguliwa na kunyanyaswa na jamii kutokana na imani potofu kuhusiana na magonjwa ya akili.

“Kwa hiyo, natoa wito kwa Watanzania wote, wasiwabague watu hao kwani ni jukumu letu kuhakikisha tunawahudumia na kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kupunguza unyanyasaji dhidi yao,” alisema Mndeme.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wagonjwa wa Akili ya Mirembe, Erasnus Mndeme, alisema kwa siku wana kawaida ya kupokea wagonjwa 12 wenye matatizo ya akili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles