30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo miaka 61 ya uhuru-Simbachawene

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema nchi imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa maendeleo ambayo ni shirikishi na yamelenga watu.

Waziri Simbachawene ametoa kauli hiyo Desemba 9, mwaka huu katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara kilichofanyika Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

“Katika ujenzi wa maendeleo ukisema ujenzi wa sekondari za kata, vituo vya afya, barabara vyote vimetekelezwa kwa kushirikisha wananchi,” amesema Simbachawene.

“Kauli mbiu ya miaka 61 ya uhuru: Amani na Umoja ni nguvu ya maendeleo yetu.” Imetusaidia kutimiza shabaha zetu. Mabadiliko ya kisiasa, mabadiliko ya kiuchumi, Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amepeleka maendeleo hayo kwa watu na maendeleo ya watu yanahitaji rasilimali fedha,” alisema Simbachawene.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene akikabidhi vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika uandikaji wa insha kuhusu miaka 61 ya Uhuru.

Sisi Watanzania tuna misingi yetu kila awamu inayoingia inategemea misingi ya awamu iliyopita ndio maana tumefika hapa tulipofika.

 “Watanzania wanapenda furaha, watanzania hawapendi hofu, watanzania ni watii kwa mamlaka, tuendelee kuheshimiana na kuipenda nchi yetu,” amesema Simbachawene.

Amesema hata wenye mawazo mbadala Rais Dk Samia amefungua mipaka ndio sababu anazungumzia R-nne ili watu wawe na utaratibu wa maridhiano; maelewano, kujenga upya, na kuendelea mbele.

“Tunaiona Tanzania iliyobadilika sana kimaendeleo, lakini imebakia na misingi ile ile iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu katika mioyo ya watu,” amesema Simbachawene.

Tulivyopata uhuru falsafa ya Baba wa Taifa (Julias Nyerere) alisema, Uhuru ni kazi ndio maana wananchi wamejikita katika kufanya kazi.

Awali, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, George Fuime alisema nchi imepiga hatua kwenye miundo mbinu ya Mawasiliano.

Naye muwasilishaji mada Mwl. Charles Malugu amesema Serikali ya awamu ya sita imefanya ujenzi wa sekondari vyumba 20,000 na ujenzi wa vyumba 3,000 kwa shule shikizi ambao utasaidia wanafunzi wa kidato cha kwanza na wanafunzi wa darasa la kwanza kuanza masomo bila kuwa na kikwazo cha aina yoyote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles