31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Tanzania ifanye nini kuvuna faida za huduma ya afya kwa njia ya mtandao?

Katika miaka ya hivi karibuni, mapinduzi ya teknolojia za kidijitali yamekuwa mengi. Hii imezipa nchi nyingi faida bunifu za kupambana na changamoto mbalimbali.Mfano wa faida hizo ni huduma za afya kwa njia ya mtandao (m-health).

Kwa watoa huduma za afya wengi, m-health imeleta njia mpya za namna ya kutoa huduma ya afya kwa wahitaji. Kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya Deloitte, m-health ina tija kwa wote, wagonjwa na watoa huduma kwa wagonjwa. Mfano, mgonjwa anaweza kutumia mtandao kuperuzi dalili za ugonjwa na kushirikisha wengine ili kupata tiba stahiki.
Jinsi ambavyo ukuaji wa teknolojia na matumizi ya simu unaongezeka, idadi ya watu wanaotumia na kufaidika na m-health nayo itaendelea kuongezeka. Wataalamu wa sekta ya afya na teknolojia wanasema kwamba Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kufurahia matunda ya maendeleo haya ya kiteknolojia katika sekta ya afya.

Mfano, mgonjwa anayeweza kusoma vyema dalili za ugonjwa wake kwa njia ya mtandao anaondoa ulazima wa kwenda hospitali kwa baadhi ya matatizo. Katika eneo jingine, jumbe fupi za simu (SMS) zimesaidia kuwapa kina mama wanaonyonyesha taarifa sahihi kuhusu lishe kwa watoto wao.
Wakati tunafurahia teknolojia hizi na tija katika maisha yetu, ni vyema kukumbuka mchango mkubwa wa kampuni za mawasiliano ya simu ambazo zimetuwezesha kufikia maendeleo haya kwenye m-health. Mbali na kuweka miundombinu sahihi ya huduma hizi kukua, kampuni za simu pia zimeendelea kuwa bunifu kuwezesha wateja wake kupata huduma hizo.
Tigo Tanzania, mmoja ya kampuni kubwa za mawasiliano ya simu za mkononi nchini inawapa wateja wake, huduma hizi za m-health kama bima za afya na maisha. Huduma kama hizi zinaonesha namna gani kampuni hizi zinajiongeza na kwenda mbali zaidi kuhudumia wateja wake kwa ubunifu.

Tigo pia imewezesha usajili wa vizazi kipitia njia ya mtandao na hivyo kuwezesha upatikanaji wa haraka wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto. Hii ni hatua muhimu kwani cheti cha kuzaliwa ni nyaraka muhimu na ya awali kwa maisha ya binadamu yeyote ili kuweza kupata huduma zinazofuatia maishani kama afya, fedha, na kadhalika.
Tukiendelea kufurahia mchango huu wa kampuni za simu katika kuleta tija kwenye maisha yetu, tuendelee kuzijengea mazingira bora ya kufanya kazi hapa nchini Tanzania na kuziunga mkono ili ziendelee kufanya kazi bora zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles