22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

TanTrade yawajengea uwezo wajasiriamali Temeke

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wajasiriamali wanawake 50 kutoka kutoka vikundi mbalimbali katika Wilaya ya Temeke wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo waweze kutambua fursa za masoko zilizopo ndani na nje ya nchi.

Mafunzo hayo ambayo yametolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kwa kushirikiana na Shirika la Posta ni mwendelezo wa mafunzo yaliyofanyika Visiwani Zanzibar Machi 8 wakati wa kilele cha Siku ya Wanawake duniani.

Wajasiriamali kutoka Wilaya ya Temeke wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tantrade).

Akifungua mafunzo hayo Meneja wa Uendelezaji wa Biashara ndogo na za kati kutoka TanTrade, Crispine Luanda, amesema wamejipanga kuwaendeleza wajasiriamali wadogo na wa kati waweze kutumia fursa zilizopo ndani na nje ya nchi.

Amewataka wajasiriamali hao kuondoa woga katika kufanya biashara kwa kushirikiana na kuwakaribisha katika mamlaka hiyo waweze kutatuliwa changamoto za kibiashara.

“Ukitaka kufika haraka nenda peke yako lakini ukitaka kufika mbali zaidi nenda na wenzako,” amesema Luanda.

Naye Ofisa Biashara (Uendelezaji biashara ndogo na za Kati), Deo Shayo, amesema mbinu za kukuza masoko ni pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa na kuhudhuria katika maonesho mbalimbali ya biashara ili kutanua masoko na kupata uzoefu wa kibiashara, kujisajili na kuuza bidhaa kupitia maduka mitandao ambayo kwa Tanzania yanasimamiwa na Shirika la Posta Tanzania.

Kwa upande wake Ofisa Masoko kutoka Shirika la Posta Tanzania, Rose Mafuru, amesema wajasiriamali wanaweza kunufaika na huduma zinazotolewa na shirika hilo kama vile Duka Mtandao (E-Shop) ambapo mfanyabiashara anaweza kuuza bidhaa yake kokote duniani na kuwaongezea mapato na kukuza biashara zao.

Mmoja wa wajasiriamali kutoka Soko la Stereo, Jackline Richard, amewashukuru waandaaji wa mafunzo hayo ambayo yamewajengea uwezo na kujiamini, kujua fursa zilizopo pamoja na kugundua mbinu mpya za kibiashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles