30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TanTrade, Tcdc kushirikiana kuunyanyua ushirika

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) zimesaini makubaliano ya kushirikiana kuwawezesha wanaushirika kupata masoko endelevu.

Makubaliano hayo yenye lengo la kuwawezesha wana ushirika na wakulima kupitia vyama vya ushirika nchini kuzalisha bidhaa zao kwa tija ili kufikia masoko endelevu yametiwa saini katika Ofisi za Tume zilizopo jijini Dodoma na kushuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Latifa Mohamed Khamis na Mrajisi wa tume hiyo, Dk. Benson Ndiege.

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa amebainisha kuwa progamu hiyo inalenga kuongeza thamani za bidhaa za ndani na kisha kuwaendeleza wazalishaji na hatimaye waweze kuwa na uwezo wa kutumia fursa za biashara na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kwa Upande wake Dk. Ndiege amevisihi vyama vya ushirika nchini kuhakikisha vinashiriki kikamilifu katika programu zilizoainishwa katika makubaliano hayo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali za kuleta mabadiliko kwenye uchumi wa nchi.

Pande zote mbili kwa pamoja zimeridhia kuwa na mabadiliko ya kasi katika sekta ya biashara ili kwenda sambamba na Serikali ya Awamu ya Sita inayohimiza uongezwaji wa thamani kwa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini ili kuwaletea wananchi maendeleo yenye tija.

Makubaliano hayo yanalenga ushirikishwaji katika programu za TanTrade za kukakikisha bidhaa za vyama vya ushirika zinapatiwa masoko endelevu ambapo wanachama wa vyama hivuo watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles