29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tanrods yatakiwa kukamilisha ujenzi Rusumo-Lusahunga

Na MWANDISHI WETU-KAGERA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Masiliano, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, ametoa siku Tatu kwa Uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kagera,  kuhakikisha wanakamilisha ukarabati wa barabara ya Rusumo – Lusahunga (KM 92) ambayo imekuwa kero kubwa kwa wasafirishaji wa mizigo ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza jana wakati wa ukagauzi wa barabara hiyo, , Mwakalinga, alimtaka Kaimu Meneja wa mkoa na wasaidizi wake kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana kuanzia leo ili kuruhusu magari ambayo yameshindwa kupita kuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

“Nadhani meneja umenielewa, nataka ndani ya siku tatu kama ulivyoahidi barabara hii iwe inapitika, na hakikisheni mnafanya kazi usiku na mchana kuanzia leo ili mkamilishe kazi hii,” alisema Mwakalinga.

Aidha, Mwakalinga ameongeza kuwa barabara hiyo inatakiwa kuwa yenye viwango bora kutokana na umuhimu wake katika uchumi wa nchi, na hivyo kumuelekeza Mkurugenzi wa barabara wa Sekta hiyo Mhandisi Hussein Mativila, kuhakikisha wanatazama kwa jicho la pekee na kuzipa kipaumbele barabara zote ambazo zinaunganisha nchi yetu na nchi jirani.

Mwakalinga, amefafanua kuwa barabara hiyo imetengewa kiasi cha Sh bilioni 12.5 ambazo ni kwa ajili ya kuwekewa lami ambapo kwa kuanza ameelekeza utekelezaji wa fedha hizo uanze kwa kurekebisha vipande vilivyoharibika sana.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa (TANROADS) Mkoa wa Kagera, Mhandisi Jackson Lwerengera, amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kukamilisha ukarabati wa barabara hiyo ndani ya siku alizowaagiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles