30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TANROADS yatakiwa kukamilisha mradi Missenyi

Na Renatha Kipaka, Karagwe

Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) imetakiwa kusimamia kukamilika kwa wakati ujenzi wa daraja la Kitengule ili kufungua fursa kwa Wananchi wa Wilaya ya Karagwe na Missenyi mkoani Kagera.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Miundombinu, Moshi Kakoso juzi akiwa na wajumbe wakati wa kutembelea daraja hilo lenye urefu wa Km 140 ambalo linaunganisha mawasiliano yawWakazi wa Missenyi na Karagwe.

“Tanroad mjitahidi kukamilisha mradi huu kwa wakati ili uweze kufungua fursa kwa wananchi wa wilaya ya Karangwe na Missenyi,” amesema Kakoso.

Awali, Menejea TANROADS mkoani Kagera Mhandisi Yudas Msangi alisema, ujenzi huo ulianza Oktoba 2018 na kutarajiwa kukamilika Mei, mwaka huu.

Msangi amesema katika daraja hilo kuna barabara unganishi zenye urefu wa Km 18 ambao bado unaendelea na umefikia asilimia 36.8.

Amesema mradi huo upo nyuma kwa asilimia 2.92 kutokana na matatizo yaliyojitokeza ikiwamo kuchelewa kuundwa kwa hati ya msamaha, kuondolewa ongezeko la thamani na mvua kunyesha juu ya wastani.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya amesema Februari mwaka huu, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbalawa alipita katika barabara unganishi na daraja la Kitengule na kutolea maagizo “Barabara unganifu zijengwe kwa kiwango cha rami” na sasa ipo kwa zaidi ya asilimia 80.

Aidha Mradi huo unathamani ya bilioni 30 ambapo serikali imetoka Bilioni 25 na kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar imetoa bilioni 5 ilikusaidia katika ujenzi huo.

Hata hivyo, daraja la Kitengule linajengwa kwa lengo la kuunganisha barabara juu ya Kyaka, Bugene, Benako, Karagwe na Ngara mkoani Kagera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles