24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Tanga, Mtwara kipimo cha FM Academia

fm academia-wazee -official imageNA MWALI IBRAHIM

BENDI ya muziki wa dansi nchini ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, imesema kukubalika kwa nyimbo zao katika ziara ya kimuziki waliyoifanya mkoani Tanga na Mtwara zimetoa mwanga mzuri kuelekea katika uzinduzi wa nyimbo zao mpya na albamu yao kwa ujumla.

Msemaji wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alitaja nyimbo zao mpya kuwa ni ‘Dada wewe’ na ‘Moyo wangu’.

“Nyimbo zetu zimeanza kufanya vizuri kwenye mikoa hiyo na tuna imani zitafanya vizuri kuelekea katika onyesho letu maalumu litakalofanyika sikukuu ya Pasaka Ukumbi wa Arcade, uliopo Mikocheni.

“Kwa sasa tunaendelea kukamilisha nyimbo zitakazokamilisha albamu yetu ambayo tutaizindua muda wowote baada ya kukamilika lakini katika onyesho letu la Pasaka kuna nyimbo mpya tutawaletea mashabiki wetu,’’ alisema Mkinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles