30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tanga Cement kuendelea kudhamini Kili Marathon

Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Uongozi wa kiwanda Tanga Cement umeahidi kuendelea kudhamini mashindano ya Kimataifa ya mbio za Kilimanjaro Marathon ili kuendelea kuleta ufanisi zaidi na kufungua fursa kwa wanariadha.

Akizungumza na waandishi wa habari Februari 22, 2023 Meneja wa Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa Tanga Cement, Justice Kanju amesema kuwa mbio hizo zimekuwa zikileta hamasavkubwa ndani na nje ya nchi na kwamba kama mmoja wa wadhamini wataendelea kushirikiana na waandaaji wa mashindano hayo.

Amesema kiwanda kampuni ya Tanga Cement itaendelea kuunga mkono mashindano hayo kwa kuendelea kuyadhamini iliyaweze kuleta tija zaidi.

Mashindano hayo ni chachu kubwa kwa maendeleo ya Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla kupitia kuutangaza utalii wa Mlima Kilimanjaro pamoja na vivutio vingine mbalimbali vya utalii.

Amesema lengo la kampuni hiyo kudhamini mashindano hayo ni kuiunga mkono Serikali katika juhudi zake zinazolenga kukuza uchumi wa Taifa kupitia michezo.

“Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon zimechangia kwa kiasi kikubwa kukuza utalii wa michezo na hii imesaidia sana serikali katika azma yake kukuza sekta ya utalii nchini na sera ya Taifa ya utalii na sisi kama wadau tupo tayari kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,”amesema.

Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon huandaliwa na taasisi ya kimichezo ya Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa hapa nchini na kampuni ya Executive Solutions Ltd.

Mwaka jana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim majaliwa aliwaagiza waandaji wa mbio za Kilimanjaro Marathon kupandisha hadhi na kuipa jina Kilimanjaro International Marathon kutokana na mbio hizo kushirikisha mataifa yote duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles