23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TANESCO yaonya mafundi wasio na leseni

MWANDISHI WETU-NJOMBE

SHIRIKA la umeme Tanzabnia (TANESCO), Mkoa wa Njombe limewataka mafundi umeme wasiokuwa na leseni ya EWURA ya kutoa huduma hiyo kukata ili kuweza  kudhibiti mafundi vishoka ambao wamekuwa wakitoa huduma hiyo kinyume cha sheria.

IRIKA la umeme Tanzabnia (TANESCO), Mkoa wa Njombe limewataka mafundi umeme wasiokuwa na leseni ya EWURA ya kutoa huduma hiyo kukata ili kuweza  kudhibiti mafundi vishoka ambao wamekuwa wakitoa huduma hiyo kinyume cha sheria.

Agizo hilo limetolewa jana na Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Njombe, Mhandisi Yusuph Salim, katika mkutano mkuu wa umoja wa wakandarasi na mafundi umeme mkoani humo (UMAU).

Alisema shirika limefikia hatua hiyo kutokana na majanga ya nyumba nyingi kuungua moto unaotokana na shoti ambazo zinasababishwa na dosari za ufundi wa vishoka na kudai kwamba mafundi hao wasio na sifa watadhibitiwa kwa kupitia leseni hizo ambazo zinatolewa kwa kuzingatia vigezo vya EWURA.

Awali akitoa taarifa katika mkutano huo, Mwenyekiti wa UMAU, Willy Mtewele  alisema licha ya jitihada zinazochukuliwa na TANESCO nchini katika kuwadhibiti vishoka lakini bado kuna mafundi ambao wamekuwa wakiwaibia wateja.

Pamoja na hali hiyo baadhi ya wakandarasi na mafundi akiwemo Kandidasti Patta, Oresta Mgaya na Johnson Otalu walisema mgongano wa kimasilahi baina ya pande zote tatu ndiyo zimekuwa chanzo cha kutokea kwa vishoka.

Walisema endapo kila mtu angefanya kazi kwa kuzingatia mipaka yake jambo hilo lisingetoa kutokana na kuwapo kwa miongozo ya TANESCO.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles