24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Tanesco yakutana na wenye viwanda kanda ya kati

Grace Kisyombe

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO), limefanya mkutano na wateja wake wakubwa na wenye viwanda katika Kanda ya kati, kikao hicho kilihusisha wawekezaji wenye viwanda katika mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida.

Akifungua rasmi mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amesema  serikali iliahidi kuwapatia Watanzania huduma ya umeme iliyo bora na yenye uhakika ili kuweza kuwakwamua kiuchumi wananchi hususan walioko maeneo ya vijijini.

Dk. Mahenge ametaja miradi midogo na mikubwa inayoendelea mkoani humo ni pamoja na ule wa uboreshaji wa kituo kikubwa cha gridi cha Zuzu ambacho kinaongezewa uwezo  kutoka uwezo wa kupokea megawat 48 hadi kufikia Megawati 400, kazi ambayo inafanywa na serikali  kwa ushirikiano na mdau wa maendeleo ambaye ni African development bank.

Dk. Mahenge  amewaomba wawekezaji kutumia fursa hiyo ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kuwekeza zaidi katika viwanda mbali mbali hasa ikizingatiwa kuwa Dodoma sasa ndio Makao Makuu ya Serikali.

Naye Meneja Mwandamizi Tanesco Kanda ya Kati, Mhandisi  Athanaius Nangali amesema wana miradi mingi inayoendelea katika maeneo mbali mbali ya Kanda ya kati, akiitaja miradi hiyo ni pamoja na ule wa upanuzi wa Kituo cha kupoza  umeme  cha Singida  kutoka Megawat 32 hadi kufikia uwezo wa Megawati 400.

“Kwa Mkoa wa Dodoma kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa ‘Ring circuit’ ya njia ya usafirishaji umeme itakayo jengwa kutokea Kituo cha Zuzu hadi Kituo cha Msalato, kuelekea Ihumwa katika mji wa serikali, kutokea hapo Ihumwa njia hiyo itakwenda mpaka maeneo ya Kikombo, ambapo pia kutakuwa na kituo cha uwezo wa 220/33kv  na njia hiyo itaunganisha kikombo hadi Zuzu,” amesema Nangali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles