29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Tanesco yaita wawekezaji Arusha

Bakari Kimwanga, Arusha

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limewataka wawekezaji nchini kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya kuwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda kwani umeme upo wa kutosha.

Akizungumza leo Jumanne Januari 22, mjini hapa, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Mhandisi Herini Mhina, amesema uzalishaji huo umeongezeka kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali kwenye miradi mbalimbali ya umeme.

Amesema uwekezaji huo umeliwezesha shirika hilo mkoani humo kutoa huduma za uhakika kwa wateja wakubwa wa umeme, wa kati na wadogo bila usumbufu wowote.

“Tanesco Arusha tunakaribisha wawekezaji wengi zaidi waje kuwekeza kwenye sekta mbalimbali, tuna umeme wa kutosha, tunaamini viwanda ni njia ya kutupeleka katika uchumi wa kati,” amesema Mhandisi Mhina.

Amesema Serikali kupitia Tanesco imetekeleza miradi mingi ya umeme, jamii haifahamu uwekezaji uliofanyika ambao ni mkubwa na wenye gharama kubwa.

“Eneo la Loliondo-Samunge, Tanesco wanazalisha umeme megawati tano ambao unatokana na jenereta zinazotumia mafuta ya dizeli,” amesema.

Akizungumzia hali ya kukatika umeme, amesema kwa sasa tatizo hilo halipo kabisa, umeme hukatwa yanayofanyika matengenezo na ukataji miti ili kusafisha njia za umeme.

“Kwa sasa mkoa huu unazalisha umeme wa megawati 120 ingawa mahitaji kwa sasa ni megawati 75 jambo linalifanya Tanesco kuwa na bakaa ya umeme wa megawati 50.

“Uwekezaji uliofanywa na serikali katika sekta hii, umemaliza tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kama ilivyokuwa miaka ya nyuma,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles