27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TANESCO YAELEKEZA SABABU KUKATIKA UMEME

Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji
Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji

Na FERDNANDA MBAMILA, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), limesema kukatika kwa umeme kila wakati kunasababishwa na uboreshaji wa miundombinu katika maeneo mbalimbali husika, hususani katika Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji,  alisema suala la kukatika kwa umeme  linatokana na kuboreshwa kwa miundombinu ya umeme kwa kuweka mipya.

“Lakini pamoja na maboresho hayo, kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara, kama shirika huwa tunaomba radhi kwa wananchi kabla ya kukata ingawa  tatizo hilo linakuwa nje ya uwezo wetu,” alisema Laila.

Alisema hata hivyo kabla ya kukata umeme, shirika hutoa taarifa kwa umma kwa njia mbalimbali ikiwemo matangazo kupitia vyombo vya habari nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles