26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Tanesco: Msitumie mafundi wa mitaani kuunganisha umeme

Na Raymond Mihayo-Kahama

WANANCHI wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wametakiwa  kutumia wakandarasi wanaotambulika na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), kuunganisha nishati ya umeme majumbani na viwandani ili kuepukana na ajali za umeme.

Ajali za umeme zinaweza kutokea na kuhatarisha maisha ya watu na mali zao maeneo hayo, kama ufungaji wa miundombinu utafanywa na mafundi wa mitaani.

Hayo yalisemwa juzi na Mhandisi Mkuu Idara ya Utafiti wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Aurea Bigirwamungu, wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kutoa elimu kwa watumiaji wakubwa wa umeme na wa kati katika Kijiji cha Segese.

Alisema wanatakiwa  kuwa na matumizi bora ya nishati ya umeme kuepuka ajali, ikiwa sambamba na kuboresha na kulinda mali zao kwa usalama.

 Bigirwamungu alisema shirika linatambua mafundi ambao wamesajiliwa na Ewura.

“Ajali nyingi za umeme zinasababishwa na mafundi wasio na leseni wanaofanya kazi hizo, pengine maafa.

“Lakini kama watafanya wanaotambulika ikitokea ajali ni rahisi kuchukuliwa hatua na kuwawajibisha,” alisema Bigirwamungu.

Alisema shirika lipo kwa ajili ya kutoa miongozo ya utumiaji salama wa umeme na kuacha kufunga kamba za chuma kwenye makenchi  na kuwatahadharisha wananchi kuhusu upitishaji wa nishati chini ya ardhi na kuunganishiana kiholela kwani inaweza kuleta maafa ya kuua watu pale nyaya zinapochunika.

Ofisa Mkuu wa Masoko, Monica Massawe alisema Serikali inawekeza katika uzalishaji wa umeme na kuimarisha miundombinu yake ili wateja wawe na matumizi bora.

Mmoja wa wananchi, Hosea Kajuna  alilitaka shirika kusambaza umeme haraka maeneo ambayo hayana nishati hiyo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles