26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Tanesco mbioni kuja na mita za kisasa

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) limesema liko katika majaribio ya mita za umeme ambazo mteja ataweza kulipia na kuingia kwenye mita husika moja kwa moja kama inavyofanyika kwenye ving’amuzi.

Hayo yamesemwa Jumatano Februari 22,2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa shirika hilo, Martine Mwambene wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya shirika hilo.

Amesemwa waliahidi kuwa Agosti mwaka jana wawe na smart mita ambazo zinamwezesha mteja kununua na kuingiza umeme moja kwa moja kama ilivyo kwenye king’amuzi.

Amesema wanaangalia teknolojia iliyobeba vitu vingi na gharama ambayo itaweza kuhimilika kwa mteja.

Amesema kuna majaribio yanaendelea kufanyika ya baadhi ya mita na itakayokuwa bora zaidi ndio itakayotumika.

Mwambene amesema wao hawauzi umeme na kuwa wanachouza wao ni huduma wanazozitoa.

“Yapo mazingira ambayo mteja amekuwa akigharamia nguzo zaidi ya sita, sheria inaruhusu namna ya kumfidia na anafidiwa kupitia wateja watakaounganishwa katika eneo hilo. Lakini inatumika zaidi katika miradi,”amesema.

Amesema kwenye mteja kugharamia nguzo tatu ni gharama za kawaida ambazo ziko katika utaratibu wao wa malipo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,405FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles