30.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Tanesco kulipa fidia ajali za moto

tanes oNA ESTHER MNYIKA, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco)  kupitia Kitengo  Afya na Usalama Kazini, limesema litaendelea kulipa fidia  kwa wateja  ambao  wanapata ajali za moto zilizosababishwa na shirika hilo baada ya kufanya uchunguzi.

Mbali na hilo, Tanesco limewataka wateja wake kuhakikisha wanaunganishiwa umeme na mafundi au wakandarasi waliosajiliwa na shirika hilo ili kupunguza ajali za moto.

Meneja wa Afya na Usalama Kazini  wa Tanesco,  Mhandisi  Majige Mabulla, alisema Dar es Salaam jana kuwa kuna kesi nyingi za ajali za moto kutoka kwa wateja wao, lakini kabla ya kulipa fidia wanafanya uchunguzi kama kweli chanzo ni shirika lenyewe na wakibaini mteja analipwa fidia ndani ya miezi mitatu.

Hata hivyo, alisema katika kesi 100 za ajali ya moto, mbili tu ndiyo hubainika kuwa chanzo chake ni Tanesco, lakini nyingine zinasababishwa na sababu tofauti ikiwamo kuwasha mishumaa, kuweka godoro karibu na swichi za umeme na vinginevyo.

Mhandisi Mabulla alisema kuwa matukio ya moto yanayosababishwa na umeme hutokea kutokana na kuzalishwa kwa joto kali ndani ya nyaya kunakosababishwa na umeme kuwa mkubwa kuliko uwezo, kulegea kwa maungio ya nyaya pamoja na radi au nyaya za umeme kuangukia juu ya paa la nyumba.

“Katika utafiti niliofanya  kuhusu ajali za moto mwaka 2009 hadi mwaka 2013, kesi  123 zimesababishwa na Tanesco na nyingine zinasababishwa na vyanzo vya vitu mbalimbali  tunavyotumia majumbani,” alisema.

Aidha Mhandisi Mabula alisema wateja pia wanapaswa kuhakikisha mfumo wa umeme unapitiwa upya kila baada ya miaka mitano pamoja na kuwa makini katika utumiaji wa vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles