24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

TanEA: Uchaguzi serikali za mitaa ungeunganishwa na uchaguzi mkuu

Brighiter Masaki

Mashirika yasio ya kiserikali ya Action for Change (ACHA) na The Right Way (TRW) yaliyoungana ili kutoa elimu ya mpiga kura, urai na uangalizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, imeshauri uchaguzi huo kufanyika sanjari na uchaguzi mkuu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu  Desemba 02, Mkurugenzi wa Ufundi (TanEA), Wallace Mayunga amesema malengo yao yalikuwa ni kuchangia katika uchaguzi ulio huru, haki, uwazi, usawa na kuaminika.

Amesema malengo mengine ni pamoja na kutoa elimu ya uraia na mpiga kura, kuangalia uchaguzi hususani mwenendo na maandalizi kabla ya mchakato wa uchaguzi, uandikishaji, kampeni, upigaji kura, kuhesabu kura na hatimaye kutangaza matokeo.

“Mapembekezo yetu ni kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa ufanytike  sanjari na u chaguzi mkuu, kwa vile imedhihirisha kuwa hamasa katika uchaguzi huo ni ndogo uikilinganisha na uchaguzi Mkuu unaochagua rais, wabunge na madiwani.

“Lakini ikiwezekana hili lifanyiwe kazi katika uchaguzi ujao wa  2025 mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2020, kwani wananchi wengi wanadhani uchaguzi wa Serikali za mitaa hauna umuhimu,” amesema Mayunga.

TanEA  ilifanya uchunguzi huo baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI), ambapo ilifanya uangalizi katika mikoa (13) ya Tanzania Bara na wilaya arobaini (40) kama zilivyoambatanishwa kwenye kiambatanisho jumla ya Watazamaji 150 walisambazwa katika wilaya na mikoa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles